Kufatia ukaguzi ambao ulifanywa kwa agizo la IGP Camilius Wambura kama sehemu ya kudhibiti wimbi la ajali nchini Jeshi la Polisi Tanzania limebaini vyuo 161 vimefanya udanganyifu kwa kutoa mafunzo ya udereva ambayo haya kidhi vigezo na kuvifungia vyuo hivyo
Zoezi hilo la uhakiki lilianza January 02,2023 katika vyuo vyote vya udereva Tanzania nakugundulika vyuo vilivyohakikiwa ni 297 na vyenye sifa ni 134 amesema IGP
“Umefanyika pia ukaguzi wa leseni 20,944 ambazo zimehakikiwa ni sawa na 1.3%, kati ya hizo leseni 17,726 za Madereva zimebainika kuwa na sifa na wamepewa barua ya udhibitisho”alisema IGP Wambura
Pamoja na hayo leseni 3,214 za Madereva zimefutiwa madaraja kutokana madereva wa leseni hizo kuwa hawana sifa ya kuwa na madaraja C na E kutokana na sababu za kutosomea madaraja stahiki hii ndio sababu ya kupatikana kwa madereva wasio kuwa na viwango na kusababisha ajali.
Leave a Reply