Vitu vya kuangalia ukiwa unanunua simu

Vitu vya kuangalia ukiwa unanunua simu

Kila mtu anatamani kuwa na simu nzuri na mpyaaaa… Whether hiyo simu ni brand ya Apple, Samsung, Tecno ama yeyote ile, kila mtu anataka kitu kilicho bora.

Leo nakuletea list ya vitu ambavyo unatakiwa kuvizingatia ama kuviangalia pale unapotaka kununua simu mpya. Hata kama hiyo simu unayonunua ni used au refurbished, hakikisha unacheck hivi vitu kabla haujapigwa:

BATTERY HEALTH

Jambo la kuangalia kwenye settings ni battery health. Make sure unaona neno lineandikwa “battery health” na ina features kabisa.

Pia usisahau kuangalia asilimia ya hiyo battery health, kama simu ni mpya kabisa, inatakiwa iwe 100% na kama imetumika basi jitahidi usinunue simu ambayo battery health yake ni chini ya 90% au imeandikwa “battery needs service” kwani utakuwa umepigwa vibaya mno.

SERIAL NUMBER

Kwenye settings pia upande wa general, bonyeza about, kuna kitu utakutana nacho kinaitwa “Serial number na model number,” hakikisha zipo na ukiweza ziingize kwenye (apple serial number/ Apple model number) simu ya apple itakuambia ni simu gani.

Bila hivyo vitu ndugu yangu, basi jua tu umepotea njia na simu hiyo ni feki!

STORAGE

Je hua unaangalia simu unayoinunua ina uwezo wa kutunza vitu kwa ukubwa gani? Hii inasaidia sana kama wewe ni mtu wa mambo mengi. Hakikisha unanunua simu yenye storage ya juu, walau 64GB ili uweze kuenjoy simu yako. La sivyo, kila baada ya kupiga picha kadhaa au kudownload apps chache, simu itakuambia imejaa afu uanze kuhangaika.

SPEAKER

Hujawahi uziwa simu ambayo ukajikuta kila ukiongea hausikiki? Basi bosi wangu uliuziwa simu yenye matatizo ya speaker.

Kila ukinunua simu, jaribu kuitest na kuona kama speaker na mic zinafanya kazi. La sivyo zile voice note za WhatsApp unazopendelea kuzituma zitakuwa zimeishia papo hapo. 

CAMERA

Jambo jingine la muhimu sana ni camera.

Kama wewe upo kama mimi, basi kupiga picha ni kitu muhimu sana kwenye Maisha, hasa Maisha ya mitandaoni. 

Ukitumia taka kununua simu, mfano iPhone 13, camera hakikisha ina cinematic mode kama sio itatoa vizuri kwa iphone kubwa na nenda kaangalia hata software update kwenye settings ukienda kwenye general utaona imekuambia iko ios ngapi, Kama ni copy huwezi ukaona haya.

Kingine ukizingatia upande wa camera angalia kama ina mwanga wa blue ambayo inaashiria ndani hakuna camera, lakini pia jaribu hata camera zake kwani kwa iPhone 13 hata usiku inapiga picha vizuri sana kwani ina Night Mode, Zingine zinajitahidi tu.

UZITO

Hili sasa linaweza kukushangaza kidogo kwani watu wengi hawakujua kuwa simu zinatofauti katika uzito.

 

Simu ni feki hata ukiangalia muonekano wake ni tofauti kabisa na genuine phone kwa ambae hujawahi shika, genuine kabla hujanunua simu jitahidi uwe na mtu anaezijua simu ili uepuke kuibiwa.

Lakini pia genuine phones ni nzito kuliko simu hizo copy, kimuonekano hata ukiona copies huwa ni flat sana.

VIFAA VINGINEVYO (ACCESSORIES)

Simu nyingi huwa inakuja na accessories zake ili kuisaidia simu yako kutokuharibika kwa haraka. Accessories hizi ni kama vile chaji na earphones. Ingawa kwa miaka ya hivi karibuni tumeona kampuni kadhaa kama Apple wakipunguza accessories kwasababu wanaviuza kivyake, ila hakikisha hivi vitu vipo kama vinapaswa kuambatana na simu yako.

Mara nyingi kuvinunua tofauti huwa ni fake kabisa.

Sasa ndugu yangu kuwa mjanja. Hakikisha kabla haujanunua simu mpya umevifuatilia hivi vitu kwa umakini mkubwa sana ili kuepukana na kuingizwa mjini.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags