Vita ya Israel na Palestina yamponza Ghazi

Vita ya Israel na Palestina yamponza Ghazi

‘Klabu’ ya #Mainz ya nchini Ujerumani, imemsimamisha mchezaji wao, Anwar El Ghazi, baada ya ‘kuposti’ katika #Instastory yake akionesha kuunga mkono Palestina.

Mchezaji huyo wa zamani wa Aston Villa na Everton pia alitumia ukurasa wake wa wa Twitter kufafanua post yake ya awali, ambayo imefutwa, akisema kuwa anaunga mkono na kuwaonea huruma wapalestina huku akitoa wito kwa mataifa wa fahamu juu ya vita hiyo.

Kutokana na hayo mchezaji huyo amesimamishwa kufanya mazoezi pamoja na kuondolewa kikosini kwani msimamo aliochukua juu ya vita hivyo haukubaliki na ‘klabu’ hiyo.

‘Klabu’ imepanga kukutana na mchezaji huyo wiki chache zijazo ili kuamua hatua zinazofuata.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags