Vinicius Jr: Hispania ni nchi ya wabaguzi wa rangi

Vinicius Jr: Hispania ni nchi ya wabaguzi wa rangi

Nyota kutoka klabu ya Real Madrid Vinicius Jr amesema hayo baada ya mashabiki kumtolea kauli za kibaguzi wakati timu yake ikipoteza kwa goli 1-0 dhidi ya Valencia  katika Ligi Kuu ya Hispania (LaLiga)

Baada ya mchezo huo ambao Vinicius alitolewa kwa kadi nyekundu amesema "Ligi ambayo walicheza Ronaldinho, Ronaldo, Cristiano na Messi, leo inamilikiwa na wabaguzi wa rangi. ubaguzi ni kawaida La Liga, imefikia hatua kule kwetu Brazil inajulikana wazi Hispania ni nchi ya wabaguzi wa rangi” amesema Vinicius

Kocha wa Madrid Carlo Anclotti, amesema mchezo ulitakiwa kusimama kutokana na vitendo vya kibaguzi vilivyofanywa hadharani dhidi ya mchezaji wake.

Huku upande wa uongozi wa La Liga umesema unapinga vitendo vya kibaguzi na utachukua hatua kwa watakaobainika kufanya vitendo hivyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags