Vilivyoongoza kutafutwa kwenye mtandao wa Google 2023

Vilivyoongoza kutafutwa kwenye mtandao wa Google 2023

Mwaka 2023 ukiwa unaelekea kukatika mtandao wa Google tayari umetoka matukio yaliyoongoza kutafutwa kwenye mtandao huyo.

Google imetoa matukio hayo katika sekta mbalimbali ikiwemo kwenye habari zilizo-trend, michezo, burudani, wasanii, movies, maeneo na Tv Shows.

Katika upande wa kumi bora ya wasanii waliotafutwa sana wameongozwa na mwanamuziki Shakira, wakifuatiwa na Jason Aldean,Joe Jonas, Smash Mouth, Peppino di Capri, Gino Paoli, Tom Kaulitz, Kellie Pickler, José Luis Perales na Anna Oxa.

Upande wa movie zilizoongoza ni Barbie, Oppenheimer, Jawan, Sound of Freedom, John Wick: Chapter 4, Avatar: The Way of Water, Everything Everywhere All at Once, Gadar 2, Creed III, Pathaan.

'Timu'za soka zilizotafutwa zaidi kwenye mtandao wa google ni Inter Miami CF, Los Angeles Lakers, Al-Nassr FC, Manchester City F.C, Miami Heat, Texas Rangers, Al Hilal SFC, Borussia Dortmund

Kwenye habari na matukio kwa mwaka 2023 ni vita ya Israel na Gaza, Titanic submarine, tetemeko la ardhi nchini Uturuki Turke, vita Sudani. Kwenye upande wa vifo vya watu maarufu waliongoza kutafutwa kifo cha Matthew Perry, Tina Turner, Sinéad O'Connor, Ken Block na wengineo.

Aidha games zilizongoza kutafutwa ni Hogwarts Legacy, The Last of Us, Connections, Battlegrounds Mobile India, Starfield, Baldur's Gate 3, スイカ ゲーム, Diablo IV, Atomic Heart na Sons of the Forest

 

Kati ya hivi vitu kipi umewahi kukitafuta kupitia mtandao wa Google?
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags