Vifo vya tetemeko la ardhi Uturuki na Syria vyafikia 36,000

Vifo vya tetemeko la ardhi Uturuki na Syria vyafikia 36,000

Zoezi la uokoaji likikaribia mwisho idadi ya watu waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea Jumatatu iliyopita nchini Uturuki na Syria imeongezeka na kufikia zaidi ya watu 35,000.

Maafisa kutoka mamlaka ya udhibiti wa majanga ya Uturuki wanasema watu 31,643 wamefariki nchini humo, huku kaskazini magharibi mwa Syria kwa sasa idadi hiyo ikifikia 4,300 kulingana na maafisa wa Umoja wa Mataifa. Inaleta jumla ya vifo vilivyothibitishwa hadi 35,943.

Umoja wa Mataifa unasema vifo hivyo henda vikaongezeka zaidi kutokana na zoezi linaloendelea na kuvuka idadi ya watu 36,000.

Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA, Martin Griffiths anasema awamu ya utafutaji manusura inakaribia kufikia tamati hivi karibuni, kuruhusu maafisa kujielekeza kuwapa manusura makazi muhimu, chakula, shule na kuwaweka sawa kisaikolojia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post