Utajiri wa Diddy ni balaa

Utajiri wa Diddy ni balaa

Ndiyo hivyo, hata mbuyu hufika wakati ukaanguka. Ndivyo inavyotokea kwa watu wengi. Ilianza kwa O. J. Simpson, Bill Cosby, R Kelly na wengine wengi na hasa wakihusishwa na kesi za unyanyasaji wa kingonohao wote ni Wamarekani weusi.

Sasa imeibuka kwa mkali wa Hip Hop na mmiliki wa lebo ya muziki ya Bad Boy Entertainment, Mmarekani mwingine mweusi, Sean Love Combs ‘P Diddy’ ambaye kwa sasa yupo mahabusu akisubiria kuanza kusikilizwa kwa kesi zake kadhaa zinazomkabili.

Kama ilivyo kwa mastaa waliotajwa hapo juu waliotumikia na wanaotumikia kifungo pamoja na wengine, wamefanya kazi kubwa kwenye muziki na kutengeneza pesa nyingi za kuwawezesha kutamba kokote, kuwekeza kwenye biashara na mambo mengine.

Diddy ni mmoja wa mastaa waliofanya makubwa kwenye muziki na kutengeneza pesa ndefu na mara kadhaa amekuwa akitajwa na Jarida la Forbes kama msanii wa Hip Hop tajiri zaidi duniani, akichuana na mastaa wengine kama Jay Z, Dr Dre, Kanye West na wengine.

Asilimia kubwa ya pesa zake anapata  kupitia muziki na kwa mwaka 2022 pekee aliingiza Dola 50 milion zaidi ya Sh100 bilioni, pia kwa wastani tangu alipoanza muziki hadi sasa kila mwaka alikuwa akikunja zaidi ya Dola 60 milioni kutokana na uuzaji wa albamu zake na malipo ya shoo.

Pia ana kampuni yake ya kudizaini na kutengeneza nguo iitwayo “Sean John,” aliyoianzisha mwaka 1998. Diddy pia ndiye bosi wa kampuni ya Combs Enterprises, inayojihusisha na uwekezaji kwenye biashara mbalimbali.

Ukiondoa hiyo pia alikuwa ana hisa kwenye kampuni ya viwanywaji ya Ciroc vodka na televisheni ya Revolt TV.

Akishirikiana na wafanyabiashara mbalimbali aliwahi kuinunua kampuni ya Aquahydrate, mwaka 2019 na kuwa mwekezaji mkuu wa kampuni ya PlayVS.

Amewahi kuigiza katika  muvi mbalimbal kama Made (2001), A Raisin in the Sun (2008), Get Him to the Greek (2010), Draft Day (2014) na The Defiant Ones (2017), huko anakadiriwa kupata zaidi ya Dola 20 milioni katika muvi zote.

Hadi mwaka 2023, alikuwa na utajiri unaofikia Dola 1 bilioni ambao unamfanya kuwa msanii tajiri zaidi wa kiume kwenye Hip Hop  baada ya Jay Z.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags