Utafiti: Wanaotumia gharama kubwa kwenye harusi, hupeana talaka mapema

Utafiti: Wanaotumia gharama kubwa kwenye harusi, hupeana talaka mapema


Kwa mujibu wa utafiti uliyofanywa na Hugo M Mialon (Profesa, Idara ya Uchumi, Chuo Kikuu cha Emory) na Andrew Francis-Tan (Lecturer wa Shule ya Sera za Umma ya LKY) kutoka Marekani unaonesha kwamba wanandoa wanaotumia pesa nyingi kwenye harusi zao wana uwezekano mkubwa wa kupeana talaka baadaye kuliko wanandoa ambao wametumia gharama ndogo.

Utafiti huo uliowahushisha wapenzi na wanando takiribani 3,000 umebaini kuwa wanaonunua pete za uchumba dola 2,000 hadi 4,000 ikiwa ni zaidi ya Sh 5 hadi 10 milioni wanauwezekano wa asilimia 1.3 ya kupeana talaka ikilinganishwa kwa wale wanaotumia dola 500 ikiwa ni zaidi ya Sh milioni 1 kuwa na uwezekano mdogo wa kutalikiana.

Hata hivyo katika upande wa bajeti ya harusi imebainishwa kuwa wapenzi wanaotumia chini ya dola 1,000 ikiwa ni zaidi ya Sh 2.7 milioni wana kiwango cha chini cha kupeana talaka ikilinganisha na wale waliotumia bajeti za harusi inayozidi dola 20,000 sawa na 54 milioni wanauwezano mkubwa wa kutalikiana.

Aidha imeeleza kuwa wanaotumia dola 10,000 na 20,000 wana asilimia 26 ya uwezekano wa kutalikiana huku wanaotumia kiasi kidogo cha fedha kwenye bajeti wana asilimia 53 za uwezekano wa kupeana talaka.

Mbali na hayo watafiti hao wameweka wazi kuwa wanawake wanaofanya sherehe za ziada zinazogharimu zaidi ya dola 20,000 (Sh 54 milioni) wana uwezekano wa 1.6 zaidi wa kupewa talaka.

Chanzo tovuti ya wanasheria kutoka Marekani Schlaich & Thompson.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags