Utafiti: Asilimia 52 ya wahitimu wanafanyakazi ambazo hawajasomea

Utafiti: Asilimia 52 ya wahitimu wanafanyakazi ambazo hawajasomea

Kulingana na ripoti iliyotolewa na kampuni ya utafiti wa data ‘Burning Glass Institute and Strada Education’ imeeleza kuwa asilimia 52 ya wanafunzi waliohitimu Degree nchini Marekani wanafanya kazi ambazo hawajasomea (hazihitaji elimu ya chuo kikuu).

Ambapo kufuatiwa na ripoti hiyo imebaini kuwa ndani ya mwaka mmoja hadi mitano ya kuhitimu na kukosa ajira, wahitimu hao huchukua uamuzi wa kufanya kazi ambazo hawajasomea zikiwemo, uhudumu wa chakula, usaidizi katika ofisi, wafanyausafi, ujenzi, pamoja na kujishugulisha na biashara.

Ripoti hiyo, iliyotolewa siku ya juzi Alhamis imezua gumzo kupitia mitandao ya kijamii baada ya kuona idadi kubwa ya wahitimu wakifanya kazi ambazo hawajasomea.

Hata hivyo waandishi wa ripoti hiyo walimalizia kwa kuwashauri wanafunzi kuelewa mapema hatua za kuchukua ili kupunguza kukosa ajira pindi watakapo hitimu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post