Usijizeeshe kwa vipozi visivyofaa

Usijizeeshe kwa vipozi visivyofaa

Habari msomaji wa fashion, ni wiki nyingine tena tunakutaka hapa ni kiamini kuwa u mzima wa afya tele na unaendelea na masomo pamoja na majukumu yako ya kulijenga taifa hili.

Leo tunakutana ili kuelezana na kujuzana mambo mbalimbali kuhusiana na masuala ya mitindo, urembo na mavazi ambayo najua huwenda unayajua ila mimi nakujua tu zaidi.

Basi katika masuala ya urembo tutaangalia vipondozi vinavyofaa kwa wanawake na mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kujiremba ambayo kama ukijafanya basi hautaonekana mzee.

Wote tunafahamu kuwa urembo ni kauli maarufu sana na hivyo inatokana na ukweli kwamba wanawake wengi hasa wa mjini wanapenda kujiremba.

Hata hivyo katika kujiremba uko wengi wao wamekuwa wakikosea katika kujipamba huko jambo linalowafanya wanaonekana vituko mbele ya jamii badala ya kuvutia.

Yapo makosa mbalimbali ambayo wanawake wengi wanayafanya wakati wanapojipodoa hali ambayo uwafanya wasiwe na mvuto tofauti na matarajio yao.

Makosa hayo ni kwamba wanawake wengi utumia vipodozi visivyofaa na ambavyo haviendani kabisa na rangi ya ngozi zao jambo ambalo akipaka uonekana mzee na sio wa kuvutia tena. 

Wanawake wengi wamekuwa wakitumia kioo tu kujiridhisha kuwa wamependeza kwa namna walivyojipambana kwa vipodozi vya aina mbalimbali.

Lakini yapo mambo ambayo mwanamke akiyafanya yanazidisha urembo wake mfano akizipendezesha kope zake, rangi ya mdomo, akipata makeup inayovutia na kuendana na rangi ya ngozi yake pamoja na marashi, manukato au unyunyu kama wanavyoita vijana wa mjini.

Leo tunaangalia kwa uchache mambo ya kuzingatia wakati kujiremba.

Nafahamu kuwa wanawake wengi wa mjini sasa hivi wanapenda kubandika kope bandia katika macho yao lakini wengi wao wamekuwa wakikosea kujua kope sahihi zinazowafaa.

Watu wanafikiri kupandika kope ndefu ndiko kunamfanya mtu kuonekana vizuri jambo ambalo si kweli unapaswa kuchagua kope yenye urefu wa wastani kisha uzibandike machoni kwako.

Ni muhimu kumpata mtaalam anaweza kuzibandika kope hizo kwa usahihi na si mtu wa kubahatisha kwani usipobandikwa vizuri ni hatari kwa afya ya macho yako.

Hata hivyo tunajua kuwa zipo aina ya rangi mbalimbali za kupaka kwenye kope lakini zinatofautiana hivyo ni vyema kabla ya kupaka ukawasiliana na wataalamu wa mambo ya urembo kwa ushauri na siyo kukurupuka kwani unaweza kupaka rangi ambayo ukaonekana kituo mbele za watu. 

Rangi ya mdomo nayo ni eneo lingine linalompendezesha mwanamke ila ukweli ni kwamba tunatofautiana sana midomo ambayo wazungu wanaita ‘lips’.

Kila mwanamke ana tofautiana midomo na mwingine kwahiyo hata rangi ya midomo nayo inakwenda sambamba na aina ya lips na rangi ya ngozi ya mwili aliyo nayo siyo unajisiriba rangi ya mdomo halafu unaonekana kituko.

Pia lipo suala hili la makeup hapa ndipo kwenye tatizo kidogo, wanawake wengi hawajui kabisa rangi sahihi za makeup wanayopaswa kuipaka, nashauri tu kabla ya kupaka ni vema ukamtafuta mtu anayevijua vitu hivyo.

Aidha natambua kuwa marashi au unyunyu ni muhimu sana kwa mwanamke lakini ni vyema nikaweka angalizo kuwa haipendezi kwa mwanamke kupulizia manukato yanayonukia sana mpaka yakawakera wengine hivyo ni vyema wakajilipuzia marashi yenye staha yasiyokera.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags