UNTOUCHABLE: Rapper anayepambania muziki wake

UNTOUCHABLE: Rapper anayepambania muziki wake

Ebwana eeeeh!!! Daaah hivi unajua ili uwe mwanamuziki wa Hip-Hop unatakiwa ufahamu vitu gani haswa vya msingi? Je unajua kuwa unatakiwa uwe mbunifu, lakini pili uwandishi wa mistari unahusika hapa, yaani content ile mistari ya kufikirika bhana, bila kusahau freestyle ni muhimu pia.

Hivyo ndivyo wakali wa hizi mambo wanavyotuelezwa bhana, chukua hiyo tembea nayo au sio? Its furahi day, leo kwenye makala ya michezo na burudani namleta kwako mtu mbadii, myamwezii kutoka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).

Hapa namzungumzia mkali wa Rap, Andrew Andrew maarufu kama  UnTouchable, akiwa mwaka wa pili, akisomea Bachelor of Mechanical Engineering, akiwa kijana anayefanya muziki wa Rap, mwenyewe wanaita kuchanaaa.

Aiseee UnTouchable kuchana umeanza lini?

“Mziki wa Rap nimeanza zamani sana. Tangu nikiwa darasa la nne nilikuwa nafanya shows kwenye graduation za shule nilikuwa nafanya sana ndipo nilipoanzia huko?

Ili mtu afanye muziki wa Hip hop anatakiwa ajue vitu gani?

“Cha kwanza kabisa ili mtu awe bora ni uandishi wa mistari yani kustick kwenye mada moja halafu pia punch line, mawazo extra yani kuwe na vitu vya kufikirika kwani ukiwa na vitu hivyo vinakupa uwanja mpana wa kuweza kuexpress your feelings kwenye mada husika”anasema.

Why hujaimba bongo flev, singeli au hata taarabu umechagua rapper

“Niseme tu binafsi yangu Hip hop is my life ndo kitu ambachonakipenda na nakifanya nimetoka nao mbali sana, singeli, taarabu na mingine ni miziki mizuri ila kwako mimi hip hop ndiyo first choice”anasema.

Je muamko wa wasanii wa Hip Hop nchini unauonaje?

“Muamko wa wasanii nchini sio mbaya tofauti na zamani tukiangalia wasanii wa hiphop wanafanya na wasanii wengine tukiamuangalia  John Makini ambaye alifanya collabo na chidinma kwenye nyimbo yao ya Perfect Combo unaona kabisa hapo jinsi tunavyotoka hadi nchi za jirani pia kama Kenya” anasema nakuongeza

Je Rapper inalipa kweliii?

“Rap inalipa asilimia miamoja na mimi nishuhuda kwenye hilo mimi ni upcoming lakini tayari ni juzi tu hapa nimefanya challenge ya Infinix ambayo mshindi wakwanza hadi watatu alipatiwa zawadi”anasema na kuongeza

“Mimi nilikuwa mshindi watatu nikabahatika kupata dolla mia 500 sawa na  shilingi milioni moja na kitu hivi  pamoja na simu ya infinix note 10  yenye thamani ya laki tano na elfu sitini rap ibnalipa bwana” anasema.

Msanii gani wa Hip hop unamkubali?

“Khaligraph johns kutoka Kenya namkubalisana na kwa hapa kibongo bongo young killer ile ngoma ya ‘Shorts’ kati ya young killer na curry ndiyo ngoma yangu bora kabisa milele na milele”anasema.

Changamoto kubwa kwenye hip hop ni ipi?

“Changamoto ni nyingi sana ila kubwa ambazo mimi naziona ni hizi hapa jinsi tunavyochukuliwa kwanza tunaonekana tunafanya muziki mgumu  wasanii wa hip hop watu wanaona kama sisi hadi tutumie madawa, bangi ili tupate stimu ya kuandika mistari yetu lakini sio hivyo wajue kuwa sisi ni wasanii kama walivyo wengine”anasema na kuongeza

“Wasanii wa hip hop hawapati support kwenye kazi zao hata ukiangalia matamasha mengi sana ambayo yanaandaliwa unakuta wanaita wasanii wa muziki mwingine wakiwa wakutosha tu lakini kwa upande unakuta anaalikwa mmoja tu hiyo nayo ni changamoto kubwa mnoo”anasema.

Jamiii inauelewa muziki wa hip hop?

Yap jamii inauelewa muziki wa hip hop coz always hip hop its abaout reality inazungumza ukweli wanajamii wanapenda kusikiliza mashairi, ubunifu kwenye ile mistari na ule ukweli unaotolewa kwenye mistari unasikilzwa sana kwenye jamii pia”

 Malengo Yako ni yapi Kwenye kipaji Chako na masomo?

Malengo yangu kwenye Hip hop ni kuja kuwa Rapper mkali yani mtu akisikia Un Touchable zero one basi hajiulizi mara mbili mbili yaani ananijua, lakini kwenye masomo yangu ndoto zangu zinatimia nilikua na ndoto zakuwa engineer ndicho ninachosemea kwa sasa”anasema.

Hivi kitu gani unakichukia maishani mwako?

“kitu kikubwa ninachokichukia kwenye maisha yangu nidharau yani mtu kumdharau mtu au kitu anachokifanya hii kitu siipendi sana maishani namuomba Mungu nisimdharau mtu na wala nisidharaulike ni kitu ambacho nakichukia sana “anasema.

Kipi ni kipaumbele kwenye maisha Yako?

“Kipaumbele change ni Mungu kwanza kwani namuamini sana yeye kila ninachokifanya lazima nimtangulize yeye hivyo Mungu kwangu ndiyo kipaumbele kikubwa sana”anasema.

Changamoto unazopitia kwenye muziki wako?

“Changamoto kubwa ninazozipitia ni Support kama unavyojua sehemu nyingi zinasupport vijana lakini nimewahi kwenda kwenye management Fulani sitaitaja jina lakini sikuweza kuambilia kitu naamin kama ningepata fursa ningekua mbali kupitia kipaji change kwani najiamini kwenye kazi”anasema na kuongeza

“Changamoto nyingine ni yakiuchumi kama unavyojua muziki unahitaji investment kubwa sana kama unavyoona mambo ya shoot yanagharama hivyo nashindwa kufanya kitu kikubwa na kizuri zaidi kutokana na masuala ya kiuchumi”.

Mafanikio?

“Namshukuru Mungu mwaka 2020 kwenye mashindano ya wanavyuo wote Tanzania wenye vipaji yaliyokuwa yanaitwa University Award niliibuka mshindi wa Best hip hop Artist ambayo yalifanywa na Uni Awards, lakni pia kwenye mashindano ya Uni Award nilifanikiwa kuingia robo fainali nashukuru”.

Je matarajio yako ni nini?

“Ni kuhakikisha jamii inayonizunguka siku moja ije ifaidike na hiki kitu ambacho ninakifanya nataka jamii ukubali kuwa hip hop inalipa na wasanii wake wako vizuri kama wasanii wengine hilo ndiyo kubwa ambalo nalipambania”.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags