Unamkomesha vipi mtu anayechungulia sms zako kwenye daladala

Unamkomesha vipi mtu anayechungulia sms zako kwenye daladala

Kila binadamu ana siri zake ambazo hapendi watu wengine wazifahamu, lakini kumekuwa na baadhi ya watu waliogeuka kero kwenye usafiri wa umma (daladala) kwa kuwa na tabia ya kusoma sms za abiria wengine.

Mara nyingi tabia hii imekuwa ikifanywa na baadhi ya abiria wanaokua wamesimama kwenye daladala kwa kukosa 'siti', uhalisia tabia hiyo inakera na kumnyima raha mtu anayesomewa sms zake, tena wakati mwingine humlazimu mtu kutumia mbinu mbalimbali kwa ajili ya kuficha sms zake.

Wapo baadhi ambao hutumia mbinu kama kupunguza mwanga wa simu,au kuweka maandishi madogo ili sms zao zisionekane.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags