UNAIKUMBUKA MAISHA NA MUZIKI YA DARASSA

UNAIKUMBUKA MAISHA NA MUZIKI YA DARASSA

Niaje mwanangu mwenyewe wa MwananchiScoop, hope huko poua kabisa na unaendelea vema na majukumu yako ya kila siku.

Leo kwenye Throw Back Thursday (TBT) tupo na mnyamwezi ambae alipoanza tukajua ameokota almasi mchangani ila kama masihara ametoboa na kufika mbali.

Huyu si mwingine ni Thabit Ramadhani maarufuku kama Darassa ambaye alifanya singo yake ya kwanza na msanii Ben Pol ambayo ilikwenda kwa jina la ‘Sikati tamaa’ waungwana kama hawakumuelewa vile ila baadae akaachia kichupa chake "Kama Utanipenda" hapa sasa mwana akajizolea umaarufu.

Niwarudishe mwaka 2017ambapo mwana alionesha maunyama zaidi na kutoa goma lake lililokwenda kwa jina la ‘Muziki’ ambalo alimshirikisha Ben Pol.

Unaambiwa kuwa kichupa chake kilikaa sana kwenye chati na kusikika maeneo yetu mengi ya kujidai, basi nikujuze tu kwa sasa kichupaa hiki kimefikisha watazamaji Milioni 19 katika mtandao wa YouTube.

Mwamba Darassa alikimbia shule akiwa bado kidato cha nne akiamini atatoboa kimziki na mpaka sasa anaendelea kuvimba kinomanoma kwenye game na kibao chake alichomshirikisha Nandy na Marioo cha Loyalty.

Utakua mjubaa sanaa kama ukiniachia comment on who You wanna see next on TBT na ngoma gani ya Darassa unaikubali sanas...Ndo kusemaaaaaaa mpaka next time wana Mwananchiscoop.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags