Umuhimu wa utunzaji kumbukumbu katika biashara yako

Umuhimu wa utunzaji kumbukumbu katika biashara yako

Huu mwaka nao nishauchoka naona kama uishe tuuu, hahahaha! I hope mko good watu wangu wa nguvu, kama mnavyo jua wafanya biashara tuko na ule msemo wetu, mali bila ya daftari huisha bila habari, usipo yatilia maanani haya maneno basi biashara yako inaweza isikue.

Utunzaji kumbukumbu za biashara hii ni moja ya kitu muhimu sana, hii ndio inaonyesha mwenendo mzima wa biashara yako ikoje utaweza kujua Kama biashara inafanya Vizuri au vibaya.

Pia kama kuna tatizo hasa kwenye  mauzo utagundua mapema, Kumbukumbu unazo weka zitatoa taarifa ya kila kitu kinacho endelea dukani kwako. Mauzo, manunuzi, madeni, na malipo yote utakayo fanya kwenye biashara yako lazima uandike kwenye daftari mimi nikupe mfano mmoja kwenye maduka Yangu ya rejereja huwa nakuwa na madaftari Kama matano. Na nakushauri nawewe uweze kuwa nayo…

  • Daftari la manunuzi

Unachotakiwa kufanya katika daftari hili ni kuandika vitu vyote ulivyonunua kwa ajili ya kuuza katika duka lako, unaandika tarehe ya bidhaa ilipo ingia dukani, jina la bidhaa, idadi yake, bei uliyo nunulia na bei ya kuuzia.

Hapa unakuwa umetunza kumbukumbu muhimu sana, mfano kama ulinunua box la sabuni, ukicheck daftari unaweza kujua kwanza faida yake ni kiasi gani kwa kuangalia bei ya kununulia, idadi ya sabuni, na bei ya kuuzia. unajua faida moja ya box la sabuni ni kiasi gani, hapa naweza piga hesabu kwa bidhaa zote ulizo ingiza dukani faida mpaka zikiisha jumla ya mauzo itakuwa ni shilingi ngapi, na hapo utajua faida ni shiling kadhaa na mtaji ni kiasi kadhaa.

Usiishie hapo hesabu hizi utakuja kuzihakiki tena katika daftari ya mauzo ya kila siku, kuhakikisha zime balance yani hela uliyo tegemea kuingiza kuanzia mzigo ulipo anza kuuza hadi umeisha ndio kiasi kile kile.

  • Daftari la mauzo


Sasa katika daftari hili unaandika kila bidhaa zitakazo uzwa dukani kila siku, tarehe, jina la bidhaa iliyo uzwa, idadi yake, na bei yake. Na mwisho wa siku una jumlishwa na inaandikwa jumla ya mauzo ya siku nzima.

Na Kumbuka hayo madaftari yote ni familia moja yanahusiana, daftari la mauzo ni muhimu sana Kama namba 1, nilivyo sema unapo fanya uhakiki lazima madaftari yote yawepo.

  • Daftari la madeni


Daftari ambalo watu wengi hawalipendio liwe katika maduka yao ila nmdo vile tuu hawana jinsi ndo biashara sasa humu unaandika bidhaa zote ambazo ziliuzwa Bila kulipiwa, yani zilizo kopeshwa.


Hapo hapo ukisha mpa mtu bidhaa kwa mkopo, Mara moja andika kwenye daftari la madeni. Jina la mkopaji, bidhaa aliyo chukua, gharama yake, na Kama ni hela nyingi mkopaji lazima aweke sahihi, na tarehe ya kurudisha Deni inaandikwa.


Hii inasaidia sana ukikopesha usisahau kudai madeni lako, mambo ni mengi unaweza mkopesha mtu , halafu wewe ukasahau angalia wakiwa watu wengi na kila Mara unasahau ni hasara kwako.

  • Daftari ya malipo


Hii nalo ni muhimu sana, unatakiwa kunaandika kila malipo uliyo fanya kuhusiana na duka,
– malipo ya pango
– Maji
– Luku
– TRA
– Leseni
– Mishahara ya wauza duka kama unao
– Malipo madogo madogo iwe hela ya ulinzi, mbeba taka, Fundi labda karekebisha umeme ulikuwa na itilafu nk


Inanisaidia kujua pia gharama za matumizi na uendeshaji duka ni kiasi gani, ukija kuangalia mwisho wa mwaka, faida uliyo ingiza na mtaji pamoja na faida utakayo pata ya mauzo hapa unaweza kujua duka unaliendesha kwa faida au hasara.

  • Daftari la mengineyo

Humu unaandika namba za simu za watu wanao kuletea bidhaa dukani soda, maji, mikate nk. uaandika tarehe ambazo utalipia kodi TRA, Tarehe za ku renew leseni na kumbukumbu nyingine na taarifa ambazo uwezi kusiandika katika madaftari mengine.

Haya haya wanabiashara wenzangu kinachotakiwa katika biashara yako inabidi uwe  makini na biashara yako hakikisha unatunza kumbukumbu zako zote, maana ni muhimu sana. Ukiskiliza maneno yangu utakuja kunishukuru badae nimekaa pale.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post