Umuhimu wa utani na masihala katika mahusiano

Umuhimu wa utani na masihala katika mahusiano

Na Habiba Mohammed
Niaje niajeeeee! Ebwana kama kawaida yetu tunakusogezea mada konki kuhusiana na mahusiano ambapo unapata kujifunza mambo kedekede ambayo kila mtu hachoki kujifunza ili kunogesha mapenzi kwa mwenza wake na uhusiano wake kuimalika.
Kama tunavyojua utani na masihala ni vitu vinavyofanyika kila siku katika  Maisha yetu pia utani ni silaha katika kuboresha mahusiano kama utautumika vizuri.
Wanasaikolojia wanasema utani na masihala katika mahusiano ni muhumimu kwa sababu zifuatazo;-

  • Utani na masihala husaidia kujua tabia ya mwenza wako

kadri mnavyokuwa mnafanya utani na masihala utaweza itambua tabia ya mpenzi wako kama ni mtu wa kukasirika haraka na kufanya maamuzi yanayo mfaidisha yeye mwenyewe.

  • Itaboresha ukaribu wenu na kila mmoja wenu kuwa muwazi

kwani mnavyofanya utani itasaidia kugundua vitu anavyopenda mpenzi wako  na kuwa muwazi kwako bila kuogopa vilevile itamsaidia kuweka wazi matatizo yake katika uwasilishaji wake.

  • Huongeza mapenzi

kwani itamfanya mwenza wako kudeka au kukudekeza kwa kukuita majina mazuri kama baby,obimo,barafu wa moyo na mengine. Chingine chakuzingatia epusha utani unaoendana na ukweli mfano, kusemea kuhusu maumbile sura nk

 Aidha utani au masihala yafanyike kwa kuheshimu heshima ya mpenzi wako ili kuepusha kugombana au kuchukia kupitia huo utani.

Aiseeee!haya wale watu ma lavu lavu nondo hiyo katika kuboresha uhusiano wako sio mtu unakuwa uko serious muda wote hadi mtu kukuita majina mazuri anashindwa, jitahidi sana kuwa karibu na mpenzi wako itakusaidia na kuwasaidia wote wawili kufikia ndoto zenu za ndoa nk.

Haya sasa mwanangu sana Dondosha comment yako hapo chini utueleze utani na masihala una nafasi gani katika mahusiano yako, au tukuache kidogo wewe ni single hahahah! Jokes






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags