Umuhimu wa logo kwenye biashara yako

Umuhimu wa logo kwenye biashara yako

 

Na Aisha Lungato

Mamboz! Siyo kila siku tufundishane kupika jamani lazima kubadilika na kuelekezana mambo tofauti ambayo pia yanaweza kukuza biashara yako, leo niko na jambo muhimu sana ambalo litakusaidia wewe mfanyabiashara ambaye unahitaji kukua kibiashara na kukuza biashara yako kwa ujumla.

Ukiachilia mbali kukuza biashara yako kupitia mitandao ya kijamii pia Logo inaweza kuwa msaada mkubwa wa kukuza biashara na kufanya uweze kuaminika kwa wateja.

Logo ni alama au nembo iliyodizainiwa mahususi kwa ajili ya biashara yako na inatumika kukutambulisha nje na ndani ya ofisi kwa maana nyingine tunaweza kusema Logo ni alama au nembo inayotumika kutambulisha huduma, bidhaa, kampuni au mfumo wowote wa vikundi.

Logo au nembo pia inamaanisha vitu vingi kuhusu biashara yako kulingana na muonekano wake, biashara nyingi sana utambulisho wake hupatikana kwanza kwenye logo, matangazo  mengi hulenga watu kukumbuka lengo na logo ya biashara.

Logo ndiyo kitu ambacho mtu hufikiria anaposikia jina la kampuni au biashara yako. Mfano, unaposikia jina Mwananchi, Mwanaspoti, The Citizen. Kitu cha kwanza kitakachokuja kwenye kichwa chako ni logo ya kampuni au bidhaa kisha matangazo uliyokwisha yasikia au kuyaona kuhusiana na huduma au bidhaa zao huanza kujirudia kichwani pindi tu utakapo yaona. Hivyo basi logo ni muhimu sana kwa maendeleo au mafanikio ya biashara yako. huu sasa ndiyo umuhimu wa Logo katika biashara yako

      Humpa mteja maana au tafsiri ya biashara yako

      Huonesha muonekano unaotakiwa

      Hukuongezea hadhi ya biashara

      Huonesha utofauti wako na wengine katika soko

      Kuwa na muonekano wa kuvutia

      Logo husaidi mteja kutamani kununua bidhaa hata kama hajaiona,

      Husaidia biashara yako kujulikana nchi nzima na katika mitandao yote ya kijamii

Kuna sababu nyingi kwa nini biashara yako iwe na logo tena siyo logo tu iwe ‘iliyodizainiwa’ vizuri.

Kutengeneza Logo nzuri siyo kufanya biashara sijui tumeelewana hapa nikiwa na maana kuwa, bidhaa yako ikiwa bora basi Logo na nembo yako itajitembeza yenyewe mitandaoni na sehemu mbalimbali kwa sababu ubora na uzuri wake katika biashara ndiyo hufanya jina la biashara yako kujulikana zaidi.

Logo mbalimbali ambazo zinajulikana nchini zimejulikana kwa sababu ya ubora na uzuri wa bidhaa zake so jitahidi katika biashara yako iwe na ubora ili uweze kupata wateja wengi kupitia hao hao wateja ulionao, bidhaa ikipendwa na mteja mmoja basi yeye ndiye atakuwa kama ambassador wako niamini kwa hili, siku hizi watu wamejanjaruka wanahitaji vitu bora na  si bora vitu, kwa sababu wanaionea uchungu pesa yao.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi

 

 

 

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post