Ukitumia ‘WiFi’ ya mtu bila ruhusa, faini tsh 23 milioni, Kifungo miaka mitatu

Ukitumia ‘WiFi’ ya mtu bila ruhusa, faini tsh 23 milioni, Kifungo miaka mitatu

Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia duniani hivi sasa mtu mmoja anaweza kutumia data ya mtu mwingine endapo tu ataunganishiwa WiFi.

Pia maendeleo hayohayo yamewezesha watu kuweka neno la siri ili kuzui watu wengine wasiweze kutumia data yao bila ruhusa, katika jamii kumekuwa na baadhi ya watu ambao wakikuta WiFi sehemu ambayo haina neno siri basi hujiunga bila ruhusa ya muhusika.

Fahamu kuwa katika nchini mbalimbali zikiwemo Marekani, Ufaransa, Uingereza, Canada, Ujerumani, Australia, na Singapore ni kosa kisheria kutumia WiFi ya mtu mwingine bila ruhusa yake adhabu hadi kifungo hutolewa.

Kwenye kufanya kosa hilo adhabu mbalimbali hutolea kulingana na sheria za nchi husika ikiwemo kulipishwa faini, na kifungo gerezani.

Kwa upande wa Singapore ukikamatwa unatumia WiFi bila idhini ya muhusika basi faini huanzia Tsh 23 milioni hadi kifungo cha miaka mitatu au vyote kwa pamoja. Hivyo watu hushauriwa kuomba ruhusa mmiliki kabla ya kutumia WiFi yake.

Tag rafiki yako ambaye asingepona kwenye hili.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags