WANANDOA wengi wameshindwa kuishi maisha ya ndoa hivyo wengi wao wamekua wanaharakati zaidi katika ndoa kuliko kuwa walezi wa ndoa zao hali ambayo imesababisha migogoro na kuvunjika kwa ndoa nyingi.
Kwa mujibu wa mtaalamu wa masuala ya ndoa Dkt Enork Mlyuka ambaye ni Muasisi na Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Marriage Child care foundation( TaMcare) anafafanua hali hii inawaathiri vipi watu walioko kwenye ndoa.
>Huathiri ustawi wa familia
>Maisha na Afya za wanandoa
>Huathiri pia watoto wao kisaikolojia na kimakuzi
>Pia huathiri ufanisi katika utendaji wa shughuli zao ama kazi zao wote wawili.
>Vile vile huathiri wazazi na familia walizotoka.
Ili kujenga misingi imara katika ndoa, na kuimarisha mahusiano ya wanandoa ili kuwa na ndoa imara zenye mvuto na uwajibikaji, wanandoa wanalazimika kupata elimu na mafunzo ya kina ya yanayohusu ndoa kabla ya kuingia kwenye ndoa.
Leave a Reply