Ukimuona, mtoto aliyetelekezwa na Mondi

Ukimuona, mtoto aliyetelekezwa na Mondi

Moja kati ya nyimbo bora zaidi kutoka kwa Diamond. Ni sehemu ya nyimbo zenye 'melodi' tamu zaidi. Ni nyimbo zile ambazo zinapendwa sana, bila kuelewa sababu ya kuipenda. Ukimuona noma.

Huu wimbo ulimkosea nini Mondi? hata kuacha ujieneze kivyake. Binafsi sijawahi kusikia mtu akiwa na maoni hasi kuhusu wimbo huu. Ajabu ni kwamba sijawahi kumjua mtayarisha husika wa ngoma hii.

'Blaza' ogopa fundi kama Christian Bella, kuurudia wimbo wako. Bella ni sehemu ya mashabiki wa Ukimuona. Kila nikitaka kusema ndiyo wimbo bora zaidi wa Mondi. Kuna sauti nasikia ikisema "Bro bakisha maneno."
Mwamba ana nyimbo nyingi sana kali. Lakini akili yangu inaamini Ukimuona ndiyo wimbo wake bora zaidi. Utulivu wa Mondi katika ngoma hii hauelezeki. Yes! alituliza kichwa, ulimi, mikono na akili.

Ukimuona ni muunganiko wa Nitarejea, Mbagala, Mawazo, Moyo wangu, Eneka na Komasava kama kifungashio. Kosa la Mondi ni kuutelekeza wimbo wenyewe. Hakuulea wala kuupamba kama zingine.

Akaacha ujitangaze wenyewe. Na hata video hakusumbuka kuufanyia. Lakini ndiyo wimbo pendwa zaidi kwa mashabiki zake. Kina Bella wameurudia lakini bado ule wenyewe ndiyo bora zaidi. Kaandika sana mule.

Tatizo mimi bado, nilipoteleza nikakosa sipajui... Mpaka akafunga virago, na akaamua kuondoka sitambui... Ubaya kinacho niumiza, maneno neno maneno... Mara kwa ndugu rafiki, kwanini anawapa misemo... Najaribu papasa...a. Kila nikitaka kusema ndiyo wimbo bora zaidi wa Mondi. Kuna sauti nasikia ikisema "Bro bakisha maneno."
Mwamba ana nyimbo nyingi sana kali. Lakini akili yangu inaamini Ukimuona ndiyo wimbo wake bora zaidi. Utulivu wa Mondi katika ngoma hii hauelezeki. Yes! alituliza kichwa, ulimi, mikono na akili.

Ukimuona ni muunganiko wa Nitarejea, Mbagala, Mawazo, Moyo wangu, Eneka na Komasava kama kifungashio. Kosa la Mondi ni kuutelekeza wimbo wenyewe. Hakuulea wala kuupamba kama zingine.

Akaacha ujitangaze wenyewe. Na hata video hakusumbuka kuufanyia. Lakini ndiyo wimbo pendwa zaidi kwa mashabiki zake. Kina Bella wameurudia lakini bado ule wenyewe ndiyo bora zaidi. Kaandika sana mule.

Tatizo mimi bado, nilipoteleza nikakosa sipajui... Mpaka akafunga virago, na akaamua kuondoka sitambui... Ubaya kinacho niumiza, maneno neno maneno... Mara kwa ndugu rafiki, kwanini anawapa misemo... Najaribu papasa...

Comments 0

Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas

Latest Post

Latest Tags