Kama ni shabiki kindaki ndaki wa msanii Marioo utagundua kuwa wakati alipokuwa akianza muziki alijulikana kupitia ngoma zake za kuumizwa na mapenzi nyimbo ambazo anazifanya kwa uchache sana.
Kwasasa msanii huyo ameonekana kubadilisha upepo jambo ambalo baadhi ya mashabiki wamekuwa wakilalamika kuhusiana na msanii huyo kuacha kutoka ngoma za kutendwa huku akibase zaidi katika nyimbo za kusifia mapenzi.
Utakumbuka kuwa Toto Bad alijitambulisha kwa mashabiki kupitia ngoma zake za kutendwa ikiwemo Inatosha, Asante, Naogopa, Raha, Aya na nyinginezo.
Malalamiko hayo yanakuja baada ya msanii huyo kuendelea kufanya vizuri katika nyimbo zinazohusiana na mapenzi hasa wimbo wa ‘Fitingi’ ambayo ameshirikishwa na Mocco Genius uliotoka siku chache zilizopita.
Baadhi ya mashabiki wameyatoa yao ya moyoni kwa kuandika “Marioo katusahau kabisa mabachela”, “Marioo tangu apate wa kufanana naye ametusahau kabisa yeye ni kutwanga ngoma za mapenzi tuu”, “Marioo naomba uimbe kama zile Dar kugumu, Yale, Inatosha, Raha yaani kule kunakasaound kako tunakamis sisi mashangazi tulikufuatilia tangu mwanzo,”
Huku wengine wakikomenti “Mzee ngoma zako zimeshadumaa mapema sana, jitahidi kubadilika kuwa star imba kama zamani hii sasa hivi ni utoto mtupu, ulikuja vizuri ghafla upo levo za Chino tena”, “Unafocus TikTok to Bro ngoma zako zinadumaa sasa hivi kwanini ulikuwa uananiaminisha kwamba utatake over saivi kwanini ngoma kama zinajirudia,”
Aidha kwa takribani mwaka sasa msanii huyo kupitia lebo yake ya Bad Nation ameamua kubadilisha upepo huku akiwekeza nguvu zaidi katika kutoa ngoma za mapenzi zikiwemo Mi Amor, Nairobi, 2025, Unanichekesha nk.

Leave a Reply