UJUMBE WA HARMONIZE WAACHA MASWALI KWA MASHABIKI

UJUMBE WA HARMONIZE WAACHA MASWALI KWA MASHABIKI

Ebwanaa mambo vipi? Mambo yanazidi kuwa moto na bila kupoa na kusogezea habari mdau wangu wa nguvu uweze kuburudika.

Aloooh! Mtandao wa Instagram umetaradadi na comment za mashabiki na story kuu iliyozua mjadala huko ni kuhusu ujumbe wa Mmakonde ambao umeacha maswali yasiyo na majibu.

Kupitia ukurasa wa Harmonize kwenye Instastory yake ameandika ujumbe ambao umeacha maswali kwa mashabiki, ujumbe huo ukiwa unasema October 10, 2022 record label ya mmakonde imeandaa sherehe kwa ajili ya kufanya maadhimisho ya miaka minne pia kuwaaga baadhi ya wasanii kutoka kwenye label hiyo.

Pia inafahamika Harmonize ndiyo mmiliki wa  record label ya Konde gang yenye wasanii wanne ambao ni Cheed, Anjella, Ibrah na Killi. Miongoni mwa swali linaloulizwa sana na walimwengu wanauliza ni wasanii wangapi kutoka konde gang ambao wanataagwa siku hiyo ya sherehe.

Mmmmh! Mmakonde katupa kitendawili kazi kwetu kutegua. Je unahisi wasanii gani na wangapi wanaondoka Konde gang? Shusha comment yako hapo chini.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Habiba Mohamed

A digital journalist and writer for mwananchi scoop My stories around entertainment,fashion, Artist profile, relationship, lifestyle and career.


Latest Post