Ujerumani yahalalisha matumizi ya bangi

Ujerumani yahalalisha matumizi ya bangi

Ujerumani imefungua njia ya kuelekea kuhalalisha ununuzi na umiliki wa kiasi kidogo cha bangi kwa ajili ya starehe. Watu wataruhusiwa kununua kiasi kisichozidi "gramu 20 na 30" za bangi kwa matumizi yao binafsi. 

Sheria hiyo hata hivyo itahitaji kupasishwa na Umoja wa Ulaya na bunge la Ujerumani kabla ya kuanza kutekelezwa mnamo mwaka 2024. Hatua hiyo imezusha mjadala mkubwa katika taifa hilo lenye uchumi mkubwa zaidi barani Ulaya, huku wakosoaji wakiibua wasiwasi kwa afya ya umma.

Waziri wa Afya wa Ujerumani Karl Lauterbach amesema kulingana na rasimu hiyo, uzalishaji na usambazaji wa bangi utaruhusiwa katika mfumo ulioidhinishwa na unaodhibitiwa na serikali.

 

Chanzo DW






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags