Ubaguzi Ulivyomtesa Tyla

Ubaguzi Ulivyomtesa Tyla

Mwanamuziki wa Afrika Kusini, Tyla amekiri kuwa amewahi kujichukia, kutokana na rangi yake kuwa nyeusi huku akitaja sababu ni kutokana na mazingira.

Alipokuwa kwenye mahojiano na ‘British VOGUE’ Tyla aliweka wazi kuwa alisoma katika shule ya msingi yenye wazungu wengi (watu wenye ngozi nyeupe), ambao walidhihaki muonekano na rangi yake nyeusi jambo ambalo lilipelekea ajichukie.

“Nilisoma katika shule ya msingi yenye wazungu wengi. Nilijichukia sana walikuwa wakiniambia tazama jinsi ulivyo mweusi sana. Na kisha nikaenda shule ya upili, ambayo ilikuwa na wanafunzi wengi Weusi na waliokuwa na utamaduni wao. Ndipo nilipoanza kujipenda na kuwa na fahari na mimi mwenyewe,” amesema Tyla

Hata hivyo, mambo yalibadilika alipohamia shule ya upili, iliyokuwa na wanafunzi wengi weusi na waliokuwa na utamaduni wao. Huko, alijifunza kujikubali na kujipenda yeye mwenyewe.

“Niko katika hatua ambayo najua mimi ni nani. Najua mimi ni mwanamke mweusi na najua mimi ni mwanamke coloured pia, na unaweza kuwa vyote viwili,”amesema Tyla

Aidha kauli hiyo iliibua mijadala mingi katika mitandao ya kijamii, huku msanii huyo akisisitiza kwamba hajatoa maelezo hayo kwa watu wanaopotosha ukweli bali ametoa taarifa hiyo kwa lengo la kuwataka watu kuanza kujikubali jinsi walivyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags