Tyson Fury na Usyk kuoneshana ubabe leo

Tyson Fury na Usyk kuoneshana ubabe leo

Bondia kutoka Uingereza Tyson Fury na bondia wa Ukraine Oleksandr Usyk, siku ya leo Mei 18, 2024 wanatarajia kupanda ulingoni kuoneshana ubabe ambapo watapigana raundi raundi 12 wakiisaka rekodi ya ‘Undisputed Champion’.

Wawili hao wanatarajia kukiwasha katika uwanja wa Kingdom Arena mjini Riyadh, Saudi Arabia, huku Mshindi katika pambano hilo akitambulika kama bingwa asiyepingwa wa uzani wa juu wa kwanza toka nafasi hiyo ichukuliwe na #LennoxLewis mwaka 1999 akimchapa Evander Holyfield.

Tyson Fury na Oleksandr Usyk ni mabondia wa uzito wa juu huku kila mmoja akiwa ameshachukua mikanda mikubwa ikiwemo WBC, WBA, IBF na WBO.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags