Tyson aanza kujifua kwa pambano lijalo

Tyson aanza kujifua kwa pambano lijalo

Baada ya kutangaza kuingia ulingoni Julai 20, mwaka huu, bondia wa ngumi za kulipwa kutoka nchini Marekani, Mike Tyson (57) tayari ameingia #Gym kwa ajili ya kuanza mazoezi ya pambano hilo.

Tyson anatarajia kuingia ulingoni na Jake Paul (27) katika uwanja wa AT&T uliopo jijini Texas pia pambano hilo litaonesha Mubashara (live) kupitia #Netflix.

Ikumbukwe kuwa mara ya mwisho kwa #Tyson ambaye ni bingwa wa zamani wa uzito wa juu aliingia ulingoni mwaka 2020, ambapo lilikuwa ni pambano la raundi nane dhidi ya Roy Jones Jr huko Los Angeles. 

Aidha kwa upande wa #JakePaul amekuwa na mafanikio kadhaa katika mchezo huo ambapo katika rekodi yake ameshawahi kuwashinda nyota wa zamani wa UFC kama Nate Diaz, Anderson Silva, Tyron Woodley, Andre August na #Bourland.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags