Baada ya kuwepo kwa tetesi kuhusiana na tuzo za Oscars kuahirishwa kufuatiwa na tukio la moto lililotokea jijini Los Angeles katika milima ya Hollywood, na sasa taarifa rasmi imetoka na kuwa tuzo hizo zitafanyika kama ilivyopangwa.
Chanzo cha karibu cha ‘Academy of Motion Pictures Arts & Sciences’ ambao wanahusika kutoa tuzo hizo wameiambia tovuti ya ‘The Hollywood Reporter’ kuwa tuzo hizo hazitaahirishwa zinatafanyika kama ambavyo ilipangwa.
"Sherehe ya Oscars, ambayo bado siku 47 tu, itaendelea kama ilivyopangwa, na wala hakutakuwa na kuongeza muda kwa wapigaji kula wala uteuzi moto unaoendelea hauhusiani na tuzo,” kilisema chanzo hicho.
Uvumi huo umezuka baada ya gazeti la udaku kutoka Uingereza ‘The Sun’ kuandika kuwa tuzo za Oscars huenda zikaahirishwa kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake miaka 96 iliyopita kufuatia na moto mkubwa unaonendelea nchini Marekani.
Moto huo unaoendelea huko Los Angeles umesababisha uharibifu mkubwa, ukiondoa maisha ya watu 25 na kuwaacha watu wengi bila makazi huku miongoni mwa walioathirika ni mastaa kama Mandy Moore, Paris Hilton na wengineo.
Tuzo za Oscars, au Academy Awards, hufanyika katika Ukumbi wa Dolby ulioko Hollywood, Los Angeles, California. Sherehe ya 97 ya Academy Awards imepangwa kufanyika Jumapili, Machi 2, 2025.
Leave a Reply