Tuzo za Grammy 2025 kufanyika Rwanda

Tuzo za Grammy 2025 kufanyika Rwanda

Inadaiwa kuwa ifikapo mwaka 2025, Tuzo maarufu duniani za Grammy zanatarajiwa kufanyika nchini Rwanda. Inaelezwa kuwa CEO wa Grammy, Harvey Mason Jr mwaka 2022 alitembelea nchini humo na kufanya mazungumo na maafisa wa Bodi ya Maendeleo Rwanda (RDB) kuhusu ushirikiano katika Tasnia ya Muziki na Sekta za Burudani Barani Africa.

Aidha kupitia ripoti hizo zimeeleza kuwa hivi karibuni tovuti ya Africa Intelligence, imetangaza miji mitano Afrika itakayo andaa Tuzo za Grammy ambapo ni Kigali, Johannesburg, Nairobi, Lagos na Abidjan.

Ikumbukwe kuwa Ijumaa Novemba 10, Grammy itatangaza vipengele vya tuzo kwa mwaka 2024 ambapo hafla ya ugawaji wa tuzo hizo kufanyika mwakani Febriari 4 katika ukumbi wa Crypto, Los Angeles nchini Marekani.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags