Tume ya uchaguzi yatuhumiwa kutokuwa na uwazi katika matokeo

Tume ya uchaguzi yatuhumiwa kutokuwa na uwazi katika matokeo

Vyama vya Upinzani vya PDP na Labor Party Nchini Nigeria vimesusia mchakato wa Utangazaji Matokeo kwa madai kuwa Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) imeonesha kuwepo kwa uchakachuaji wa Matokeo yanayoendelea kutolewa

Aidha hadi sasa ni takriban Theluthi Moja ya Kura za Majimbo 36 zimetangazwa ambapo kwa mujibu wa BBC Mgombea wa Chama Tawala (APC), Bola Tinubu ana 47% ya Kura zilizopigwa, Kiongozi wa Upinzani, Atiku Abubakar 27%, na PeterObi ana 22%

Hata hivyo, Matokeo yanayoendelea kutoka kwenye maeneo ya Kaskazini na Kusini-Mashariki mwa Nigeria yanaonekana kuwa ngome za PDP na Labour Party na kufanya Matokeo ya mwisho kutotabirika.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post