Treni zasitishwa kabla ya maandamano ya Kenya

Treni zasitishwa kabla ya maandamano ya Kenya

Shirika la Reli nchini Kenya limesitisha shughuli zake zote za treni ya abiria katika mji mkuu wa Nairobi, kabla ya maandamano ya kupinga serikali Jumatatu hii yaliyoitishwa na kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

Katika taarifa ya jana Jumapili, usimamizi wa Shirika hilo ulihusisha uamuzi huo na hali zisizoweza kuepukika "Tunaomba radhi kwa wateja wetu wote kwa usumbufu wowote uliojitokeza," lilisema

Hata hivyo mwendesha treni alisema treni zake zote za abiria kati ya stesheni ya zamani ya reli katikati mwa jiji (Kituo Kikuu cha Nairobi) hadi kituo cha reli cha Nairobi-Mombasa (Nairobi Terminus) - zitaendesha jinsi ilivyoratibiwa.

Muungano wa upinzani unafanya maandamano jijini Nairobi na maeneo mengine ya nchi kushinikiza mageuzi ya uchaguzi na kupunguzwa kwa bei ya bidhaa za kimsingi.

Siku ya Jumapili, mkuu wa polisi alipiga marufuku maandamano hayo, lakini upinzani umeshikilia kuwa maandamano hayo yatafanyika kwa mujibu wa sheria.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post