Toxic afunguka kumzimia kimapenzi Abigail Chams

Toxic afunguka kumzimia kimapenzi Abigail Chams

Msanii wa Hip-hop nchini Abdulrazak Selemani ‘Toxic’ wakati akifanya mahojianoa na Mwananchi Scoop, ameweka wazi hisia zake za kimapenzi kwa mwanamuziki Abigail Chams kwa kusema amekua akimpenda mwanadada huyo tangu miaka sita iliyopita

Toxic anayetamba na kibao cha New King kinachofanya vizuri kwa sasa, ameweka wazi juu ya jitihada alizotumia kuhakikisha anatengeneza ukaribu na binti huyo mdogo mwenye talanta kubwa ya Sanaa ya muziki

"Imenichukua miaka mingi kumpata Abby nilianza kumtumia ujumbe kwenye mitandao ya kijamii lakini nilijibiwa baada ya miaka sita bado sikukata tamaa nashukuru kwa sasa tunazungumza na mambo mazuri yanakuja,” ameeleza Toxic.

Pia msanii huyo ameonesha kumkubali mwanamuziki wa Singeli Dulla Makabila na kusifia namna anavyoweza kuandika vizuri mashairi yake huku akifika mbali zaidi kwa kusema Makabila anaandika vizuri zaidi ya baadhi ya wasanii wa Hip-hop

Mkali huyo wa mitindo huru (freestyle) pia ametoa maoni yake juu ya msanii mwenzake Young Lunya na kudai hajawahi kuelewa anachokifanya kwenye tasnia ya muziki.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags