Tiwa Savage aibukia  uigizaji

Tiwa Savage aibukia uigizaji

Mwanamuziki  kutoka Nchini Nigeria  Tiwa Savage ametangaza kuibukia kwenye filamu kwa mara ya kwanza kupitia Filamu yake aliyoipa jina la “Water & Garri’ ambayo jina hilo limetokana na EP yake aliyoiachia mwaka 2021.

Katika filamu hiyo Tiwa ameshirikiana na Director Mejia Rabi  huku maudhui makubwa ya Filamu hiyo itakuwa inamuelezea binti aneamua kurudi Nyumbani kwao Nigeria baada ya kujichimbia Marekani kwa takribani miaka 10 akijihusisha na maswala ya Mitindo.

Anaporudi nyumbani anakuta hali imebadilika machafuko, amani hakuna kama alivyoacha wakati anaondoka hivyo anajaribu kuweka mambo sawa.

Mpaka sasa haijafahamika ni lini Filamu hiyo itaingizwa sokoni, haya kibongo bongo ungependa msanii gani wa muziki aibukie kwenye uigizaji, dondosha komenti yako hapo chini mwanangu sana.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags