Tiwa avutiwa na mavazi wa Ayra

Tiwa avutiwa na mavazi wa Ayra

Wakati mashabiki kutoka Nigeria wakimshambulia mwanamuziki Ayra Starr kuhusu mavazi yake yanayo onesha maungo ya mwili, kwa mwanadada Tiwa Savage imekuwa tofauti ambapo yeye anadai kuwa anavutiwa na mavazi hayo.

Akiwa katika mahojiano yake na Kiss FM, Uingereza, ameeleza kuwa tukio hilo linalo mtokea Ayra sasa linakumbusha enzi zake wakati anaanza mziki mashabiki nchini humo walipokuwa wakimnanga kuhusu uvaaji wake.

Lakini kwa upande wake anapenda uvaaji wa Ayra huku akiyaona mavazi hayo ni ya kawaida na hayana shida yoyote inayopelekea awe ajenda kwa jamii.

Ayra Starr na Tiwa Savage wamekuwa wakishirikiana katika kazi zao za Sanaa ambapo wawili hao waliwahi kuachi ngoma kama ‘Gala’ na ‘Stamina’.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags