Titanic ya pili mbioni kutengenezwa

Titanic ya pili mbioni kutengenezwa

Bilionea maarufu kutoka nchini Australia, Clive Palmer (69) ameripotiwa kutaka kutengeneza meli mfumo sawa na Titanic iliyozama mnamo mwaka 1912 ikiwa na zaidi ya watu 2,200, inayotarajiwa kuzinduliwa rasmi ifikapo mwaka 2027.

Mara ya kwanza Palmer alitoa wazo la kutaka kujenga Titanic II mwaka 2012, ambapo mwaka huu amezindua rasmi mradi huo siku ya jana Jumatano Machi 13, katika mkutano na waandishi wa habari kwenye jumba la Opera la Sydney.

Palmer, mwenye utajiri wa dola bilioni 4.2 kulingana na Forbes, ameweka wazi kuwa mradi huo unagharimu zaidi ya dola 500 huku akijinadi kwa waandishi wa habari kuwa anapesa za kutosha hata kujenga Titanic 10.

Mfanyabiashara na mwanasiasa si mgeni katika miradi mikubwa. Yeye ni mkongwe wa sekta ya madini, mmiliki wa zamani wa klabu ya soka na alikaa katika bunge la Australia kwa miaka mitatu kati ya 2013 na 2016.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags