Tisa wafariki kutokana na mlipuko wa ugonjwa usiyojulikana, Kenya

Tisa wafariki kutokana na mlipuko wa ugonjwa usiyojulikana, Kenya

Watu tisa wamefariki na wengine zaidi ya 80 kulazwa hospitalini kutokana na mlipuko wa ugonjwa usiojulikana katika kaunti ya Marsabit kaskazini mwa Kenya.

Msimamizi wa eneo hilo alisema kati ya watu tisa ambao wamekufa, sita walikuwa watu wazima na watoto watatu kati ya mwaka mmoja na mitatu.

Wengi wa watu walioathiriwa walionyesha dalili kama za mafua, macho ya manjano, wengu kuvimba na maumivu makali ya kichwa, vyombo vya habari vya nchini humo vinaripoti.

Baadhi ya wagonjwa wamepatikana na kuwa na malaria lakini madaktari wanasema huenda ni leishmaniasis ya visceral-pia inajulikana kama ugonjwa wa kala-azar.

Aidha mlipuko huo unajiri miezi miwili baada ya Taasisi ya Utafiti wa Kimatibabu nchini Kenya kugundua mbu washambuliaji katika maeneo ya Laisamis na Saku kaunti ya Marsabit.

Chanzo BBC






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post