Tems: Ukinichumbia jua umepata ua adimu

Tems: Ukinichumbia jua umepata ua adimu

Msanii Tems amejipa maua yake kwa kudai kuwa mwanaume atakaye mchumbia au kuwa naye katika mahusiano basi atakuwa amepata ua adimu.

Mwanamuziki huyo aliyasema hayo wakati akiongea na mwigizaji #ChinasaAnukam kwenye Podcast ya ‘Is This Seat Taken’ akidai kuwa yeye ni ua adimu.

“Kuchumbiana na mimi ni kama kupata ua adimu ambalo linaonekana njeusi kutoka nje na unapolifungua, ni waridi, zambarau lakini katikati, kuna jiwe” amesema.

Tems ambaye mpaka sasa hajaweka wazi mahusiano yake lakini amedai kuwa utu wake wa nje unaweza usiwe wa kuvutia ila ndani ni mrembo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags