Tems: Namkubali Tyla na Asake

Tems: Namkubali Tyla na Asake

Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria Tems ameweka wazi kuwa wasanii anaowapenda zaidi Afrika ni msanii kutoka nchini humo Asake na mwingine kutoka Afrika kusini Tyla.

Tems ameyasema hayo wakati akiwa kwenye mahojiano ya hivi karibuni na ‘Time 100 Next Gala’ New York, baada ya kuulizwa swali kuwa ni wasanii gani wa Afrika anawapenda zaidi na kueleza kuwa ni Asake na Tyla.

Tems amerudi tena mjini baada ya ukimya wa muda mrefu ambapo kwa sasa anatamba na wimbo wake mpya ‘Me & U’ alioachia mwezi mmoja uliopita.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags