Tatizo la ugonjwa wa wasiwasi (Anxiety Disorder)

Tatizo la ugonjwa wa wasiwasi (Anxiety Disorder)

Unaweza kujiuliza wasiwasi nao ni ugonjwa eti? Basi leo ndo utajua hujui!!!

Kisaikolojia huu ni ugonjwa ambao unasumbua baadhi ya watu na kwa sasa umekuwa mkubwa kutokana na mambo ya sayansi na teknolojia.

Wasiwasi maana yake ni hisia ya kutotulia au hofu apatayo mtu katika vipindi mbalimbali, lakini pia ni majibu ya asili ya mwili wako kwa mafadhaiko.

Kwa mfano siku ya kwanza chuoni, wengi hupata wasiwasi kwa sababu ya mazingira ambayo ni mageni kwao au kwenda kwenye mahojiano ya kazi, au kutoa hotuba inaweza kusababisha watu wengi kupata hofu na woga.

Kisaikolojia hii ni hali ya kawaida kwa mwanadamu yoyote, lakini ikiwa hisia zako za wasiwasi ni kali, au hudumu kwa zaidi ya miezi sita, na zinaingilia maisha yako, itakufanya uanze kupata msaaada wa kisaikolojia.

Dalili za ugonjwa huu:

-Kuwa na hofu ya mara kwa mara

-Kukosa usingizi

Midomo kukauka

-Misuli kukaza

-Kukosa utulivu

-Ongezeko la mapigo ya moyo

Tiba ya ugonjwa huu

Kama maisha yako si ya furaha sana, ni ya msongo wa mawazo kila wakati, ni rahisi sana kuwa na wasiwasi.

Hivyo basi jaribu kufanya yafuatayo, kwani yatakupunguzia kuwa na wasiwasi na kudhibiti kupata dalili za kuwa na ugonjwa huo uliozidi.

  • Kwanza jichanganye na wengine. Upweke unaweza kukuletea au kukuongezea wasiwasi, jaribu kuyazungumzia ana kwa ana matatizo yako ya kuwa na wasiwasi, itakusaidia kuupunguza wasiwasi uliokuwa nao.
  • Jitahidi kila wakati kukutana na marafiki zako. Jaribu kuwashirikisha watu uwapendao na mambo yanayokusumbua, usiwe mpweke. 
  • Jaribu kujiepusha na mambo ambayo yanakuleta msongo wa mawazo. Unaweza kuonana na wanasaikolojia ambao watakusaidia kupunguza msongo wa mawazo.
  • Pendelea kufikiria mambo positive zaidi kuliko negative, hii itakusaidia kupona wasiwasi.
  • Jenga tabia ya kufanya mazoezi. Hasa mazoezi ya kulegeza misuli, na kuvuta pumzi kwa nguvu. Hizi ni njia za asili za kupunguza wasiwasi na msongo wa mawazo pia.
  • Kupata matokeo bora kabisa, jenga tabia ya kufanya mazoezi ya kuongeza mapigo ya moyo na kutoka jasho (aerobic exercise), kwa muda wa dakika 30 kila siku.
  • Mazoezi au shughuli za kuifanya mikono na miguu kuwa katika mwendo kwa wakati mmoja (rhythmic activities). Mazoezi haya yana manufaa sana, jaribu kutembea, kukimbia, kuogelea, au kucheza muziki wa dansi.
  • Pata usingizi wa kutosha. Kukosa usingizi kunaweza kukuza tatizo la kuwa na wasiwasi, kwa hiyo binadamu yoyote anatakiwa kulala masaa 8 ya usingizi. Jitahidi kupata usingizi, kama imeshindikana kupata usingizi, onana na wataalamu watakupatia dawa jitakusaidia kupata usingizi. 

Fuatilia suggestions hizi kwa umakini kabisa, in no time, you will be fine. Mental health ni topic ambayo huongelewa kwa uhafifu sana, take precautions, ongea na mtu!






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags