Tatizo kwenye biashara sio mtaji, tatizo ni WEWE

Tatizo kwenye biashara sio mtaji, tatizo ni WEWE

Hellow! Wanangu wa mwananchiscoop leo katika biashara tumekujia na nondo ambazo zitakusaidia katika biashara au mradi unayo taka kuuanzisha ungana nasi kupata mbinu ambazo zitakusaidia kuanza biashara ambayo itakuwa ni imara siku zote.

Watu wengi wanajua wanachopaswa kufanya hapa duniani ili kubadilisha maisha yao na kugusa maisha ya watu wengine katika jamii, lakini changamoto kubwa wanashindwa kuanza kufanya chochote kwa hofu ambayo kimsingi haina mantiki yoyote.

Hebu muulize mtu ambaye ana wazo la kufanya kitu fulani ambacho moyoni mwake anashuhudiwa kabisa kitakuwa na mafanikio,”ni kitu gani kinachokufanya ushindwe kuanza na kuishia kuongea tu?” Wengi watasingizia hawana mtaji.

Ukosefu wa mtaji ni wimbo ambao watu wengi wasiokuwa na uthubutu wanauchukulia kuwa sababu ya kuwafanya washindwe kabisa kufanya chochote na kuishia kuwa na ndoto ambazo hazitakaa zitimie.

Lakini ukiwachunguza watu wa namna hii utagundua kwamba tatizo lao sio mtaji tu bali lipo tatizo la msingi ambalo wangepaswa kulishughuliakia kwanza,kwani nini? Kwa sababu mtaji halijawahi kuwa hitaji la kwanza katika uanzishaji biashara yoyote.

MBINU ZA KUTEKELEZA MAWAZO YAKO

 

  1. WAZO

Kupata wazo la biashara, mradi au shughuli unayotaka kufanya ndicho kitu ambacho kinapaswa kuwa cha kwanza kufikiria. Kwa kutumia kipaji chako cha ubunifu ulichopewa na Mungu unatengeneza maoni ya kile unachotaka kitokee mapema kabisa.

Kupitia hatua hii unakuwa na picha ndani mwako ya namna ambavyo mradi au biashara unayotaka kuanzisha itakavyokuwa,Kwa lugha nyingine unauona mwisho tangu mwanzo na hii ni hatua ya mtu na imani.Kuna kitu ndani mwako unaamini unaweza kukibadilisha siku moja kuwa kitu dhahiri.

  1. KUANDIKA WAZO LAKO

Hatua ya pili ni kulitafsiri wazo au maoni kwenye maandishi. Kwa hatua hii unahamisha maoni kutoka picha uliyokuwa unaona pekee yako kwa macho ya ndani na sasa unaitafsiri kwenye karatasi kiasi kwamba hata mtu mwingine anaweza kusoma maoni yako.

Hatua hii itahitimishwa na kuandika mpango wa wazo lako ambayo itakusaidia kujua unahitaji nini kwa maana ya rasilimali zote zinazohitajika ili kutimiza maono yako ikiwemo muda na kuainisha vipaumbele vyako.

Hapa pia utapima nguvu uliyonayo na udhaifu wako.Na kwa kufanya mambo hayo mawili ni dhahiri kwamba umekwisha anza safari kuelekea unakotaka kufika na hapo unaweza usiwe na hitaji lolote la fedha ikiwa kila kilichopo hapo juu kiko ndani ya uwezo wako.

  1. ANZIA PALE ULIPO

Watu wengi wanashindwa kuanza kufanya chochote kwa kigezo tu cha kusubiri mpaka watakapokuwa na mtaji wa kutosha kwa kuwa hawana tu macho ya kuona thamani ya kile walichonacho mkononi. Kwa kifupi hakuna mtaji mdogo wala mkubwa mtaji wowote unafaa kuanza kitu kwa ukubwa unaolingana na nguvu yako.

Kitendo cha kuona kila fedha unayomiliki ni ndogo sana kukuwezesha kuanza kufanya biashara au mradi wa ndoto yako utachelewa kuanza mambo mengi. Kwa mtindo huu watu wengi wamezeeka na kufa bila kuanza kauishi maisha yao.

Hebu nikuulize,kama huna uwezo wa kuthamini kidogo ambacho kiko mkononi mwako unafikiri ni nani atakayekuwa tayari kukwamini kwa mambo makubwa? Haiwezekani mpaka pale utakapokuwa mwaminifu kuthamini kile ulichonancho.

 

  1. FANYA UNACHOWEZA

Huenda ikawa unatamani kuanza kwa kishindo lakini ukweli ni kwamba rasilimali ulizo nazo hazikuwezeshi kuanza kwa kishindo.Ushauri wangu ni kwamba badala ya kuendelea kusubiri kufanya unachotaka,anza kufanya unachoweza na utaona kwa kufanya hivyo utajifunza sana katika safari hiyo uliyoanza kidogo kidogo.

Kuna tofauti kubwa kati ya kutamani kufanya unachotaka na kufanya unachoweza kufanya.Kufanya unachotaka ni pale unapofanya bila kuwepo na vikwazo vyovyote na kufanya unachoweza ni pale unapofanya tu kile ambacho kiko ndani ya uwezo wako hata kama una uwezo wa kufanya zaidi.

Anza kidogo kidogo huku ukiwa na picha kubwa mbele yako ambayo unaiendea.Rudia na kurudia na utaanza sasa kupata wateja wadogo,mwisho utaanza kupata wateja wakubwa,utapata fedha na fedha yako itakua siku kwa siku.

Utaanza kujijengea heshima kwa watu na taasisi mbalimbali za fedha pia,miongoni mwao watakuja kukushauri namna gani unaweza kufanya biashara yako na kupata mtaji mkubwa ambao ulikuwa unatamani kuwa nao hata kabla ya kuanza.

Kama ni biashara sasa unajua soko,na mahitaji yako pia unayajua uwe na uhakika utakuwa katika nafasi nzuri sana ya watu kukusikiliza ukiwasilisha hoja yoyote ya kuhitaji uwezeshwaji wa fedha au raslimali zingine. Nakushauri anza bila visingizio anza.Kama biashara anza.kama ni kitu cha kipaji anza,kama ni chochote unachoaka kuanza aacha visingizo..






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags