Tatizo katika mtandao wa Whatsapp

Tatizo katika mtandao wa Whatsapp

Alooooh! Wale wenzangu wa kuweka mistatus mingi kama nawaona mnavyo zima data na kuwasha basi bwana kwa taarifa zilizo tufikia hivi punde ni kwamba mtandao huo unashida kidogo ya kimtandao dunian kote.

Mtandao wa WhatsApp hauko hewani kwa Watumiaji wengi Duniani na kufanya Watumiaje wake kushindwa kufanya chochote kwenye WhatsApp zao, sababu za kutokuwa hewani bado hazijawekwa wazi kuwa tatizo kubwa ni lipi.

Ingawa hadi sasa hakuna jibu rasmi au uthibitisho kutoka kwa Whats App, Watumiaji kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania wameripoti kwamba hawawezi kutuma au kupokea ujumbe kwenye Mtandao huo isipokuwa kwa wanaotumia WhatsApp kwenye kompyuta.

Haya wale wapenzi wa mtandao huo embu dondosha komenti yako hapo chini na utuambie ulifanya nini baada ya kuona whatsapp yako haishiki?.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags