Tapsoba amfunika Aziz Ki tuzo za Gold Stallion

Tapsoba amfunika Aziz Ki tuzo za Gold Stallion

Kiungo mshambuliaji wa ‘klabu’ ya Yanga, Stephane Aziz KI amekosa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka Burkina Faso akizidiwa kete na Edmund Tapsoba.

Tuzo hiyo imetolewa leo Juni 14, 2024 ambapo imekwenda kwa mlinzi wa Bayer 04 Leverkusen, Edmund Tapsoba.

Tapsoba alibeba tuzo hiyo ya Gold Stallion 2023 ambapo alikuwa sehemu ya kikosi cha Leverkusen kilichotwaa taji la Ligi Kuu Ujerumani (Bundesliga) bila kupoteza mchezo hata mmoja.

Leverkusen pia ilifanikiwa kutinga fainali ya Europa msimu uliopita na kukumbana na kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Atalanta.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags