Tapeli maarufu mtandaoni Hushpuppi ahukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka 11

Tapeli maarufu mtandaoni Hushpuppi ahukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka 11

Tajiri na tapeli maarufu mtandaoni Hush Puppi kutoka nchini Nigeria amehukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka 11 nchini Marekani kwa ushiriki wake kwenye utapeli wa kimataifa.

Hushpuppi, ambaye jina lake halisi ni Ramon Abbas, alidhihirisha maisha yake ya kitajiri kwenye ukurasa wake wa Instagram ambao ulikuwa na wafuasi milioni 2.8.

Aidha Jaji wa Los Angeles pia aliamuru alipe dola 1,732,841 ili kuwafidia waathiriwa wawili. Abbas atatumikia kifungo chake cha miezi 135 katika jela ya Marekani.

Hata hivyo tapeli huyo mwaka jana alikiri makosa ya utakatishaji fedha.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post