Tamasha la kuwakumbuka wasanii marehemu Septemba 7

Tamasha la kuwakumbuka wasanii marehemu Septemba 7

Kwa mara ya kwanza nchini kutakuwa na tamasha la kuwakumbuka wasanii waliotangulia mbele ya haki linaloitwa ‘Faraja ya Tasnia’ liliandaliwa na mwigizaji na Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao, Steve Nyerere.

Akizungumza na Mwananchi leo Agosti 28, 2024 Steve amesema tamasha hilo litakuwa likifanyika mara moja kwa mwaka na kwa 2024 litafanyika Septemba 7 katika Viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam bila kiingilio.



“Nimeona walikuwa wenzetu nikajitafakari kwamba familia zao zilikuwa tegemezi kwao kwa maana hiyo nikaona ni vyema kuwakumbuka tukala na familia zao na wananchi kwa ujumla siku hiyo hakutakuwa na kiingilio ni bure na kutakuwa na burudani nyingi mfano kutakuwa na bendi itakayokuwa inapiga kwa ajili ya kukumbuka nyimbo zao.

“Lakini hawatatoka mkono mtupu kuna zawadi ambazo tutawapa wafiwa pia kutakuwa na dua ambayo mchungaji Mwamposa pamoja na Shekhe wa mkoa watakuwepo na tutakula chakula cha pamoja wote hii inatupa faraja na taifa lenye amani na utulivu kwa kukumbukana na kushikamana tulichukulie hili jambo ni lamsingi sana,”amesema

Mbali na hayo kupitia chapisho aliloweka mwigizaji huyo katika ukurasa wake wa Instagram linaoesha sura za wasanii mbalimbali waliofariki dunia kama vile Mandojo, Mangwea, Bi Kidude, Mzee Majuto, Kanumba, Maunda Zorro, Sajuki, Sharobaro na wengineo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags