Swaum Mkumbi: aeleza kuhusu maisha halisi ya chuo cha NIT

Swaum Mkumbi: aeleza kuhusu maisha halisi ya chuo cha NIT

Oooooooh!!! watu wangu wa nguvu mwendo ni ule ule yaani tunaanza tulipo ishia hatunaga mba mba mba katika hili leo katika segment yetu ya unicorner, moja kwa moja tumetua katika chuo cha The National Institute of Transport (NIT) unataka kujua nini tumekipata kuhusiana na chuo hicho basi ungana nasi mwanzao mpaka mwisho…

Kama mnavyojua hatunaga iyana wala baya na mtu team ya Mwananchi Scoop moja kwa moja tukatinga katika chuo hicho tukakutana na mrembo anaefahamika kwa jina la Swaum Ramadhani Mkumbi anaechukua shahada ya rasilimali watu ( Human Resource Management).

Sasa bwana yupo hapa kutuelezea kuhusiana na changamoto wanazokumbana anzo wanafunzi wa chuo hicho…

Vijana wa chuo cha (NIT) wanakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinaweza kuwa ngumu kushughulikia. Kwanza kabisa, ugumu wa masomo ni moja ya changamoto kubwa ambazo vijana wanakutana nazo chuoni. Baadhi ya masomo ni magumu sana na hivyo kuwafanya wanafunzi kupoteza motisha na kuwa na wasiwasi kuhusu uwezo wao wa kufaulu.

Changamoto nyingine ni uhaba wa rasilimali, Chuo cha NIT Kina uhaba wa rasilimali kama vile vitabu, vifaa vya maabara, na hata vituo vya kompyuta na madarasa ya kusomea. Hii inaathiri  uwezo wa wanafunzi kujifunza na kufanya vizuri katika masomo yao.

Gharama kubwa ya elimu ni changamoto nyingine ambayo vijana wanakabiliana nayo, wengi hawana uwezo wa kulipia gharama za elimu, na hivyo kuwafanya washindwe kupata fursa ya kupata elimu bora au hata kuacha chuo kabisa.

Changamoto za kibinafsi ni pia changamoto kubwa ambazo vijana wanakutana nazo wengi wao wanakabiliana na matatizo ya kifamilia, wasiwasi, au hata matatizo ya afya ya akili.

Uvunjaji wa nidhamu ni changamoto ambayo inaweza athiri uzoefu wa kusoma na kufanya kazi kwa baadhi ya wanafunzi  huku baadhi yao wanakosa nidhamu na kufanya mambo yanayohatarisha usalama wa wenzao na hata uendeshaji wa chuo.

Ushindani mkubwa pia ni changamoto kubwa kwa wanafunzi Kuna ushindani mkubwa katika chuo kama vile ushindani wa mavazi, pesa, mapenzi na masomo ambao unafanya wanafunzi wawe na wasiwasi na hata kutokuwa na ujasiri wa kutosha. Hii inaathiri uwezo wao wa kufanya vizuri katika masomo yao na hata kujenga uwezo wa kutojiamini.

Jambo jingine ambalo liko serious kidogo bwana ni kuhusiana na pia wanafunzi wa Chuo cha NIT wanapitia changamoto za malazi kutokana na kuwa hostels ni chache wengine inawalazimu kukaa nje ya chuo (kupanga) ili kuweza kupata masomo yao, lakini huku wanapopanga wanapata changamoto ya pesa za kulipia vyumba na wakati mwingine wanashawishika na tabia za baadhi ya watu wa jamii ya nje kama kuvuta bangi, kujiuza na kuingia kwenye makundi hatarishi ili tu kutetea maisha yao.

Kwa mfano vijana wadogo wa kike wanakuwa wanajiuza ili kupata pesa wakati mwingine wanajihusisha kwenye mapenzi na watu wazima wanaoweza kuwa baba zao wenyewe wanawaita ma sponsor kwa lengo tu la kupata pesa ya kula au pesa ya kununua vitu amabavyo wasingeweza kununua kama vile simu za iphone macho matatu,nguo za bei ghali na kupanga vyumba vya bei kubwa.

Kubwa kuliko bwana ni wanafunzi/ mabinti wadogo kujishughulisha kwenye mapenzi katika umri mdogo hivyo inapelekea wao kufeli kwasababi wanahusisha mambo mawili kwa wakati mmoja unakuta mtu kaumizwa na mpenzi wake inapelekea yeye kufeli au kupata matatizo mengine ya mwili wakati mwingine wanafunzi wengine huamua kujiua wakishajigundua wanamatatizo ya kiafya, so serikali na chuo kinahitaji kuangalia maswala kama haya ili hadhi ya chuo isiweze kushuka.

Changamoto ya mwisho kabisani ya kijamii ambapo vijana wanakutana nazo chuoni vijana wanaweza kukabiliana na ubaguzi wa kijinsia, au hata unyanyasaji wa kijamii kwa baadhi yao hii inawafanya wasipende kabisa chuo na wengine kupelekea kuacha kabisa.

Kwa ufupi, vijana wa NIT na vyuo vingine vingi wanakabiliwa na changamoto nyingi chuoni, ambazo zinaweza kuathiri uwezo wao wa kujifunza na kufanya vizuri katika masomo yao. Ni muhimu kwa vyuo vya elimu ya juu kuzingatia changamoto hizi na kutoa suluhisho zinazofaa ili kusaidia wanafunzi kufanikiwa katika masomo yao na maisha yao ya baadaye.

Haya sasa hapa hatujakukataza wewe kutokusoma chuo hicho au kukatisha ndoto zako za kusoma katika chuo hicho, tulichokifanya ni kukujuza tuu yanayojiri ili hata kama ukitaka kwenda kusoma basi uwe unamachache unayajua kuhusu sehemu hiyo unapotarajia kwenda kuanzisha maisha yako mengine. Usiache kufuatilia @Mwananchiscoop ili uweze kujua mambo mbalimbali kuhusiana na vyuo mbalimbali, nasemajee tukutane tena next week halaaaaah!!!!.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post