Swael Lee aomba kuingiza verse kwenye ‘Komasava’ ya Diamond

Swael Lee aomba kuingiza verse kwenye ‘Komasava’ ya Diamond

‘Rapa’ kutoka Marekani #SwaeLee amemuomba #DiamondPlatnumz amtumie wimbo wa #Komasava’ aliomshirikisha Chley na Khalil Harrison, ili aweze kuingiza Verse (Mistari) yake.

#SwaeLee ameomba kufanya ‘kolabo’ hiyo kwa kuandika kwenye upande wa ‘komenti’ ya posti ya Diamond “Send Me That Open Verse” ameandika Swae Lee

Utakumbuka siku tatu zilizopita kupitia ukurasa wa Instagram wa #Diamond ali-share video ya Swae ikimuonesha mwanamuziki huyo wa Marekani akicheza wimbo huo ambao mpaka kufikia sasa una zaidi ya watazamaji milioni 2.7 kupitia mtandao wa YouTube.

Ngoma mpya ya Diamond Platnumz, Komasava imeendelea kuteka mioyo ya mashabiki dunia kutokana na wimbo huo kutumi Lugha kadhaa katika verse zake.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags