Style ya kusuka yeboyebo haijawahi kupitwa na wakati

Style ya kusuka yeboyebo haijawahi kupitwa na wakati

Mambo vipi wapenda mitindo kama mimi? haya sasa nikukaribishe tena kwenye ulimwengu wa Fashion hapa katika jarida lako pendwa la Mwananchi Scoop, tuweze kuudadavua urembo na mitindo mbalimbali kwa pamoja.

Leo katika Fashion bado nina jambo langu katika nywele yaani mpka mseme mmetosheka na segment ya nywele ila leo nitaenda tofauti kidogo katika kuzungumzia style ya kusuka yeboyebo za kisasa au unaweza kuita yeboyebo za Jerry, kama unavyojua mtindo huu haujawahi pitwa na wakati.

Licha ya kuzuka mitindo mipya ya nywele zilizobamba na kutufungia mwaka lakini nywele ya yeboyebo haijawahi kupoteza mvuto wake.
Kumekuwa na style nyingi za kuiboresha usukaji wa mitindo ya
yeboyebo njia mpya ambayo imekuwa ikitumiwa sana na baadhi ya wasusi ni kutumia jerry kusukia.



SWALI LA KUJIULIZA JERRY NI NINI?
Kawaida jerry hujulikana zaidi kama kimiminika chenye asili ya gundi kwa sababu ya malighafi zinazotumika kutengenezea kuwa na asili ya kunata nata. Kuna aina nyingi za jerry ambazo ni jerry laini na jerry ngumu. Katika ususi wa yeboyebo jerry inayotumika huwa ni ‘jeli’ laini.

KWA NINI WANATUMIA JERRY?
Wakati wa kusuka yeboyebo msusi huitajika kukata mistari ili mstari ukae vizuri hupaka jerry katika mstari chini ya ngozi husaidia kunyoosha vizuri mstari na kuleta mng’ao katika nywele. Pia kutumia ‘jeli’ humsaidia msusi kusuka nywele zote hata zile ambapo huwa nywele za mbele katika uso (malaika), hivyo huleta mng’ao katika uso.

Mwanamitindo wa masuala ya ususi na urembo, Mwamvi Lyaunga akizungumza na Mwananchi Scoop anaeleza njia ya kusuka yeboyebo kwa kutumia ‘jeli’ wakati wa kukata mistari ya nywele husaidia kusuka vizuri ‘rasta’ na huleta mvuto katika nywele anasema.

“Hapo awali wateja wangu nilikuwa nawasuka yeboyebo bila kutumia ‘jeli’ lakini baada ya kuzuka mitindo mingi ya nywele za ‘rasta’ zinazochambuliwa na kusukia ‘jeli’ nikaona kumbe naweza kutumia ‘jeli’ katika yeboyebo na nilipoanza kusuka hivyo wateja wangu wamekuwa wakifurahia sana kwa sababu zinawapa muonekano mzuri.”

JINSI YA KUTUNZA NYWELE ZA YEBOYEBO ZILIZOSUKWA
KWA JELI?

Nywele ni kama mmea ambao ili uweze kuota na kukua vizuri unahitaji udongo mzuri na maji, hivyo nywele yeboyebo iliyosukwa kwa ‘jeli’ ili iweze kuwa na mvuto na mng’ao lazima inyunyiziwe maji kidogo kwa mtindo wa kupulizia kama ‘spray’ kisha unapaka mafuta katika mistari na juu ya ‘rasta’.
Wakati wa kulala unapaswa uvae kofia ya nywele au kufunga kitambaa, njia hiyo husaidia kufanya nywele isifumuke pia kutochafua mashuka kutokana na mafuta ya nywele yaliyopo kichwani.

NAMNA YA KUFUMUA NYWELE YA YEBOYEBO BILA KUKATA NA KUHARIBU NYWELE
Kumekuwa na malalamiko mengi juu ya unaposuka nywele kwa
kutumia ‘jeli’ husadikika kukata nywele lakini sababu kuu inayofanya nywele kukatika ni ukavu katika nywele na sababu nyingine huwa ni nywele kutokuwa na matunzo hasa kwa kutozipa unyevunyevu na kwa wale walioweka dawa kushindwa kuzilitachi pale zinapooteana na kukaanazo muda mrefu.
Nywele yoyote isipokuwa na matunzo hukatika bila kutumia ‘jeli’ kwa hivyo matunzo ya nywele ni muhumu. Wakati wa kufumua nywele ya yeboyebo iliyosukwa kwa ‘jeli’

Unapaswa kufuata hatua ambazo zitakuwezesha kutokukata nywele na kuiacha nywele yako ikiwa na afya, kwanza unapaswa kunyunyizia majikatika nywele ya yeboyebo kisha ukihakikisha nywele imepata unyevu anza kuifumua.

Ukimaliza kufumua haupaswi kuichana utapaka mafuta
ya kimiminika kama nazi na ‘Conditioner’ ili ikuwezesha kulainisha nywele. Baada ya hapo anza kuichambua nywele kwa kutumia vidole na sio chanuo au kitana.

Ukishamaliza sasa unaweza kuiosha nywele yako kwa kutumia maji ya uvuguvugu na sabuni ya nywele (shampoo). Zikaushe nywele kwa taulo au kitambaa safi kisha paka ‘conditioner’ na mafuta laini kwenye nywele na anza kuzichana kuanzia kwenye ncha ili kutoa nywele zilizokufa.

Naseamje yaani mpaka kieleweke katika urembo wa nywele kwa sababu huo ndiyo urembo mkubwa wa mwanamke, nywele ikiwa smart, umeisuka vizuri sura nayo inaonekana jamani.

Sasa mimi this weekend niishie hapo msiombe next weend
nikapata kitu kizuri kinacho husu nywele mwendo utakuwa niuleule yaani mpka muelewe namaanisha nini but I hope next time kuna something better than hii ya leo sasa usiache kupitia jarida letu.

Yaaani mpaka usemee!!!!






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags