Soma vitabu ujiongezee maarifa

Soma vitabu ujiongezee maarifa

Ni watu wachache sana ndiyo wanaopenda na wanafahamu umuhimu wa kusoma vitabu.

Watu wengi hasa waafrika hawapendi kusoma vitabu ikiwa hakuna kinachowalazimisha kufanya hivyo kama vile mtihani kazi, kupata fedha na mengineyo.

Ukweli ni kwamba kuna maarifa mengi katika vitabu na yanaweza kuboresha maisha yao.

Moja ya faida ambayo mtu anayesoma kitabu anaweza kupata ni Kuongeza maarifa mapya.

Tukumbuke kwamba lengo linalowafanya waandishi wa vitabu kuansika ni kuweka maarifa yao kwenye mnaandishi. Hivyo kwa kusoma vitabu unapata maarifa mbalimbali yaliyoweka kwenye kitabu husika.

Hivi leo kuna vitabu vinavyohusu takriban kila kitu, kwa hiyo maarifa yoyote unayoyahitaji unaweza kuyapata kwenye vitabu.

Pia usomaji wa vitabu umfanya mtu kuweza kufikiri kwa kina, kwani unaposoma vitabu unafahamu mambo ambayo yatakufanya ufikiri zaidi, mara nyingine kitabu kitakuacha na maswali ambayo yatakufanya utafakari kwa kina zaidi juu ya mambo mbalimbali.

Inaelezwa kwamba usomaji wa kitabu umfanya mtu kuongeza uwezo wa lugha kwani ukisoma utaonbgeza kujua msamiati, kujifunza sarufi ya lugha au hata mbinu mbalimbali za matumizi ya lugha.

Unachotakiwa kuzingatia hapa ni kusoma vitabu bora mara nyingi kadri uwezavyo.

Vitabu pia hukuburudisha kwani unaweza kutembea na kitabu chochote mahali popote.

Viko vitabu mbalimbali tena vya bei rahisi ambavyo vinaweza kukuburudisha na kukufurahisha.

Vitabu hasa vile vya kifasihi ni burudani tosha ya aina yake. Unaweza kusoma vitabu vilivyochapishwa au vitabu pepe kwa kutumia simu au kompyuta yako.

Unapotumia muda wako kusoma vitabu kumbuka kuwa ni wazi kuwa hutopata muda wa kupoteza. Kusoma vitabu kutakufanya utumie muda wako kuongeza maarifa yako zaidi.

Licha ya kutokupotezea muda unaposoma vitabu pia uboresha afya yako.

Kwa kusoma vitabu upatapa maarifa juu ya mambo unayoweza kufanya ili afya yako iwe salama na bora zaidi.

Lakini pia usomaji huu wa vitabu umfanya mtu kuwa mbunifu. Kadri unavyosoma vitabu ndivyo unavyojifunza mambo mapya zaidi ambayo yatakufanya kuwa mbunifu.

Kwa kusoma vitabu pia unaweza kufahamu jinsi watu wengine walivyotumia ubunifu kutimiza malengo yao pamoja na kukabili changamoto mbalimbali.

Licha ya kwamba utapata maarifa mengi ukisoma vitabu pia unakuondolea msongo wa mawazo na hiyo inatokana na kwamba waandishi wa vitabu hujenga mazingira ambayo msomaji hujihisi yumo ndani yake.

Aidha nikujuze kwamba kadri unavyosoma vitabu ndivyo unavyoongeza uwezo wako wa kumbukumbu kwani kila mara unaongeza mambo mapya ambayo unatakiwa kuyakumbuka.

Jinsi ubongo unavyopokea mambo mapya ndivyo unavyozidi kuongeza uwezo wake zaidi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags