Snoop kupitia ukurasa wake wa Instagram ameshare picha za wasanii sita ambao ngoma zao zimekuwa zikikubalika zaidi ambao hawajawahi kushinda tuzo za Grammy akiwemo Ice Cube, Tupac, Busta Rymes, The Notorius, DMX na yeye mwenyewe huku akiandika ‘Missionary 12/13’.
Kufuatia na chapisho hili mashabiki wameibuka huku wakimpa moyo rapa huyo kwa kuandika “Grammy sio kipimo cha ukubwa kuna wasanii wengi wakubwa hawana tuzo hizo”, wengine wakiandika “Kutambuliwa mitaani ni muhimu zaidi kuliko Grammy” hata hivyo baadhi yao wametoa maoni yao kwa kuwashutumu Grammy kwa kuandika “Grammy hazithibitishi tamaduni yetu. Magwiji kama Snoop tayari wameweka historia”, “"Grammys si chochote” wameandika baadhi ya mashabiki

Utakumbuka kuwa Snoop yupo kwenye gemu kwa takribani miaka 30 huku akitamba na ngoma kama Drop It Like It's Hot, Young, Wild & Free, Sweat, Sexual Eruption na nyinginezo.
Tuzo za Grammy zinatarajiwa kutolewa Februari 2025 nchini Marekani huku rapa wa kiume ambaye ameongozwa kwa kutajwa kwenye vipengele vingi akiwa ni Kendrick Lamar.
Leave a Reply