Skales amchana wizkid

Skales amchana wizkid

Rapa wa Nigeria #Skales amemtolea povu mkali wa Afrobeats #Wizkid baada ya kudai kuwa muziki wa Hip-hop umekufa.

Skales ametoa povu wakati alipoulizwa swali juu ya Wiz kudai muziki huo umekufa katika mahojiano na ‘Hip TV’, na kueleza kuwa hawezi kusema Hip-hop imekufa kwa sababu hakuna kinacho dumu milele kila kitu kina wakati wake.

Aidha rapa huyo ameeleza kuwa ipo siku Afrobeats itakufa na kitakuja kitu kingine ni suala la muda tu ndiyo maana hata binadamu haishi milele.

“Kila kitu kitakuja na kuondoka, inamaanisha ikiwa unajoto leo, unaweza kukosa kuwa na joto kesho. Leo, ikiwa ni rap ambayo kila mtu anahisi imekufa, kesho itakuwa Afrobeats, na kesho ijayo itakuwa Amapiano, na kadhalika” alisema rapa huyo.

Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 33 amewahi kufanya ngoma kama Shake Body, Temper, Ajaga, Fire Waist, Shakushaku, Je Kan Mo na nyingine nyingi.

.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi

Comments 0

Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles

Latest Post

Latest Tags