Shule zafungwa kwasababu ya kimbunga Freddy

Shule zafungwa kwasababu ya kimbunga Freddy

Mamlaka nchini Malawi imefunga shule katika wilaya 10 kutokana na wasiwasi wa usalama baada ya Kimbunga Freddy kusababisha uharibifu katika nchi jirani ya Msumbiji.

Mvua kubwa iliyonyesha kusini mwa Malawi imesomba barabara na kutatiza uzalishaji wa umeme, huku mvua zaidi ikitarajiwa kunyesha katika siku chache zijazo.

Masomo yamesimamishwa kwa Jumatatu na Jumanne katika taasisi zote za masomo katika eneo hilo aidha walimu na wanafunzi wamehimizwa kutumia mitandaoni na redio kwaajili ya masomo, wizara ya elimu ilisema katika taarifa.

Mpaka sasa idadi ya vifo nchini Msumbiji ni takribani watu 28 tangu dhoruba hiyo ianguke kwa mara ya kwanza.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post