Shakira Zaid: Ajivunia Biashara ya kuuza nguo za Stara Mitandaoni

Shakira Zaid: Ajivunia Biashara ya kuuza nguo za Stara Mitandaoni

Na Aisha Lungato

Niaje it’s another Tuesday natumai mko pouwaa wanangu wa mwananchiscoop.

Siku ya leo bwana tunakuletea makala za biashara na kuangazia zaidi wanafunzi wanaosoma lakini huku wanajishuhulisha ili kukidhi mahitaji yao na kujikimu katika maisha.

Biashara ya kuuza nguo mtandaoni ni biashara ambayo hufanywa na watu wengi zaidi, licha ya kuwa wengine huiaribu kwa kutapeli watu lakini bado imekuwa biashara ya kidumu.

Shakira Zaid ni mwanafunzi kutoka katika chuo cha Muslim University of Morogoro ambapo anachukua kozi ya Journalism and Mass Comunication ni binti anayejishuhurisha na biashara ya kuuza nguo za stara kama vile mabaibui (Abaya) na mitandio.

Kwanini anauza nguo mitandaoni

Sote tunafahamu kuwa kila anayeamua kufanya biashara basi kuna kitu kinacho msukuma inaweza kuwa umaskini au kupenda tu kujishughulisha na vitu mbalimbali ili kujipatia kipato.

Kwa Shakira anafunguka na kusema kuwa kitu kilichomsukuma kufanya biashara hiyo kuona chuoni kwao kunauwihitaji wa nguo hizo lakini pia kuwa na hali ya kukataa kuwa tegemwezi kwa wazazi wake.

“Nilipata wazo baada ya kuona chuoni kuna uhitaji wa nguo kama hizo za stara nikahamua nianzishe biashara ya nguo hizo kwa kujua kuwa hiyo ni fursa kwangu na kama nikiitumia vizuri nitapata faida.

“Lakini pia niliamua kufanya biashra hii ili nisiwe tegemezi kwa wazazi wangu kwani nilihitaji kuwa na kipato changu mwenyewe” alisema Shakira

Changamoto anazokumbana nazo

Shakira alisema siku zote mtu akiamua kufanya biashara basi akubaliane na mambo kadhaa kama vile faida, hasara na changamboto mbalimbali.

Alisema katika biashara yake hiyo moja ya  changamoto kubwa anayoipata ni wateja kulalamika kuhusu bei na wengine ufanyiwa delivery bure lakini akifika ughahiri kuchukua bidhaa.

Faida anayoipta

Matarajio ya kila mfanyabiashara ni kupata faida zaidi ili ziweze kumsaidia katika mambo yake, lwa upande wa binti huyo yeye alieleza kuhusu faida anayo ipata “Allhamdullillah faida sikosi japo nikidogo lakini inanisaidia kukidhi mahitaji yangu madogomadogo pia inanisaidia kulipa vitu kadhaa nikiwa chuoni kama vile pesa ya pango na chakula,” alisema Shakira

Atoa ushauri kwa vijana

“Ushauri kwa vijana wenzangu wasiogope kujaribu kwasababu huu ndo umri wa kuhaso huu ndo muda wa kuhangaika hakuna muda mwengine so when ukipata nafasi wewe itumie tuu vizuri hangaika haso muda utafika wa wewe kula mema yako, changamoto hazikosekani cha muhimu ni kuweka bidii kwa kila jambo lako”amesema

Aliendelea na kueleza kuwa “Pia vijana tusiogope kujaribu kufanya jambo kwa kuhofia kuchekwa kuzarauliwa wewe fanya kitu ambacho moyo wako unakusukuma kufanya, Kingine waweze kujiongeza wasitegemee shule, watafute fursa nyingine ya kujichanganya na watu ili kupanua wigo wa maendeleo,” alisema

Mtarajio yake

Alisema anandoto za kuwa mfanyabiashara mkubwa wa nguo za stara na mpiga picha bora wa kike maarufu na kuongeza kuwa anatamani hivyo kwasababu hapendi kuajiriwa anapenda kujiajiri mwenyewe.

“Moja ya matarajio yangu ninataka kuwa mfanyabishara mkubwa wenye kuza nguo zenye ubora wa hali ya juu lakini pia nataka kuwa  mpiga picha bora mwanamke yaani femalephotographer,” alisema

Aidha alisema kuwa pia anatamani kuja kuwa kama mtangazaji wa Azam TV, Halima Shebunge.

“Mimi nasomea mambo ya uandishi wa habari hivyo licha ya kufanya biashara pia natamani siku moja nije kuwa kama Halima Shebunge ambaye ni mtangazaji wa Azam TV pia ni  mfanyabiashara na designer wa nguo za kike za stara, vyote hivyo amekuwa akivifanya kwa umakini na ubora wa hali ya juu,” alisema

Haya haya mdau na mfuatiliaji wa @mwananchischoop funguka hapo chini wewe unatamani kuwa kama nani eeeeh, umejifunza nini kutoka kwa mwanadada Shakira au tuambie unatamani kufanya biashara gani lakini mazingira hayakuruhusu kwa namna moja ama nyingine.

Tunaendelea kusisitiza kuwa usiache kufuatilia magazine ya @mwananchisoop ili uweze kujifunza mbinu mbalimbali za kibiashara.

 

 

 

 

 

 

 

 

 






Comments 1


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags